kama tujuavyo imebaki miaka miwili Rais aliyepo madarakani Jakaya Mrisho Kikwete amalize muda wake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tayari tumemsikia Rais Kikwete akijivunia utendaji wake Amesema kwamba wale walioendelea kumsema vibaya kwamba chini ya uongozi wake Tanzania haikupata maendeleo  wataoona aibu atakampomaliza muda wake. Atakuwa ameiacha Tanzania ikiwa na maendeleo yasiyo na kifani.

Ni kweli Rais Kikwete ataacha uongozi wa taifa hili nchi ikiwa na katiba mpya pia nchi ikiwa na maji safi kwa wakazi wake wengi.

 

Barabara safi zinazounganisha mikoa. Hata  hivyo inavyoonekana rais hajaona kwamba ataiacha nchi ikiwa katika hali mbaya kielimu. Ni  vyema aone hili ili achukue hatua sasa kufumua Wizara ya Elimu iliyotufikisha hapa Rais asisubiri kumaliza muda wake akiwaacha Watanzania wanapigia kelele elimu. Hii itakuwa kasoro kubwa katika  utendaji wake mzuri.

Wizara ya Elimu ina uongozi lakini kama vile haina uongozi. Pale kila mtu na lake. Wanatoa kauli zinazopingana kila kunapokucha kama tulivyoshuhudia katika sakata la alama za ufaulu mara tumefuta sifuri mara hatujafuata sifuri.


Ni kweli katika kuokoa jahazi rais ulimuteua Prof. Sifuni Mchome kuwa Katibu wa Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi


Hakuna anayetaka kuukatisha tamaa lakini kwa macho yetu wananchi hatujaona kwamba uteuzi wa Prof Mchome sana umesaidia sana kubadilisha kubadilisha mambo wizarani.


Pale tatizo si Prof Mchome. Tatizo ni Waziri wa Elimu, Dk.  Shukuru K wambwa na Msaidizi wake Mkuu, Philip Mulugo na watendaji wengine wakuu ambao Prof Mchome amewakuta wizarani. Hawana ubunifu wala mawazo yeyote yanayoweza kuisaidia kuboresha elimu Tanzania.


Huenda rais hajui hili. Watanzania wamefikia mahali ambapo wananong’onezana kwamba hawezi kumbadilisha, Dk. Kawambwa  eti ana uhusiano wa karibu. Kwa hiyo rais anaruhusu Elimu ya Umma iendelee kuvurugwa na uongozi wa  iliyomshinda kuongoza wizara hii.

 

Sina ushahidi wowote wa kuthibitisha hilo. Lakini hata kama rais ana uhusiano wa karibu na Dk. Kawambwa sidhani kwamba katikati ya  utawala bora anaouongoza angeweza kumwacha mtu mmoja anaendelee kuvuruga suala linalomgusa kila Mtanzania.

Kwa kweli rais atasaidia sana kulinda heshima za hawa watu waliovuruga elimu kiasi cha kutisha kama atawaondoa wizarani sasa.


Kusubiri miaka miwili ili amalize nao muda itakuwa kuangamiza kabisa elimu Tanzania.

Ni majuzi tu Kaimu  Katibu Mkuu Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tanzania), Zuberi Samataga, alipozindua tovuti ya ufuatiliaji na usambazaji wa vitabu vilivyotokana na fedha ya rada Hakuna mwenye neno na TAMISEMI. Inatekeleza majukumu yake.


Lakini bado tunalia na Wizara ya Elimu. Wakati TAMISEMI inafuatilia usambazaji wa vitabu hivyo Wizara ya Elimu chini ya uongozi wa Dk. Kawambwa, ilishindwa kufuatilia ubora wa vitabu hivyo kwa walimu waliovitumia kabla havijachapishwa tena.


Kwa hiyo, nimewasikia walimu wengi tu wakiponda usambazaji wa vitabu ambavyo waliviona siku nyingi kwamba ni vibovu lakini wizara haikuwasikiliza. Ikaamua kushirikiana na wachapishaji wa vitabu kuchapisha tena haraka haraka vitabu visivyofaa. Hii ni kashfa nzito ambayo katika nchi zingine asingepona mtu.


Si lengo langu kuvuruga biashara ya wachapishaji vitabu ambao Wizara ya Elimu imewahakikishia kupata utajiri kutokana na kuchapisha na kusambaza kwao vitabu vibovu.

Kwa vile nashughulika sana na masomo ya Historia na uraia binafsi nimejionea kitabu kilicho na makosa yasiyo na idadi.  Kwa mfano kitabu kimoja kinasema kwamba Merere alikuwa Kiongozi wa Wayao wa Songea.


Ukweli ni kwamba Merere hakuwa kiongozi wa Wayao Alikuwa kiongozi wa Wasangu . Tena Wayao hawapatikani Songea wanapatikana Tunduru.


Walimu wa masomo mengine wameviponda pia vitabu vya  masomo yako ambavyo vimesambazwa nchi nzima na vinasubiri mwaka mpya wa shule viendelee kuptosha ukweli wa mambo.


Hata kama hatujui ni kisi gani cha fedha kimetumika kuchapisha na kusambazwa vitabu vibovu nchini kote tunaangalia idadi ya vitabu vilivyochapishwa na kusambazwa tunaweza kupata picha taifa limepoteza kiasi gani cha fedha katika zoezi hili la kuchapisha na kusambaza vitabu vibovu nchino kote.


Tazama Education book Publishers (nakala 5,501,105 Mtule Educational Publishers (3,167,229) Ben and Company (4,608,783), Jadida Book House Ltd (1,759,479) E and D Vision Publishing (1,264,506)    Mukiki  and Nyota Publishers (605,746) Longhorn Publishers Ltd (368,702) na Best Deal Publishers (105,550).


Izingatiwe kuwa serikali imetumia kati ya shilingi elfu tano mpaka shilingi elfu kumi kununua kitabu kimoja.


Sina haki yeyote ya kudai kwamba vitabu vyote vilivyosambzwa ni vibovu. Walimua wamebaki wanalilia  vitabu ya Oxford University Press ambavyo vingi ni vizuri.


Lakini kampuni hiyo haikihusishwa na zoezi hili. Bila ya shaka kuna sababu. Basi vitabu vibovu ndiyo hivyo vimesambazwa nchini kote lakini bado serikali inahitaji kuuamba umma wa Tanzania kwa nini umevuja fedha ya umma kwa kuchapa na kusambaza vitabu ambavyo walimu wanalalamika siku nyingi kwamba ni vibovu katika mazingira hayo kwa nini Rais asiwawajibishe viongozi wa wizara kwa kashfa hii anasubiri nini kuifumua wizara


By Jamhuri