Rais Samia akutana na Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Waziri Mkuu wa  Ethiopia Mhe. Abiy Ahmed uliowasilishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mhe. Demeke Mekonnen aliyeambatana na Ujumbe wake  Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 24 April 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mjumbe Maalum ambae pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mhe. Demeke Mekonnen Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 24 April 2023.