Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan akimvalisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza (SACP) Mzee Ramadhani Nyamka Cheo kipya cha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka kuwa Mkuu wa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Majaji wa Mahakama Kuu kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka pamoja na Majaji Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu aliowaapisha Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.

By Jamhuri