Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kukabidhiwa Tuzo tatu ambazo Tanzania imeshinda katika Utalii, Afrika na Duniani. Kikao hicho kilifanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026.

Tuzo hizo zimetolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.

Muonekano wa Tuzo tatu za “WORLD TRAVEL AWARDS” ambazo Tanzania imeshinda.