Uongozi ya Hifadhi ya Ngorongoro Umefanya ziara ya kikazi kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel G. Chongolo.

Pamoja na mambo mengine walijadiliana kwa kina kuhusu Uendelezaji wa Eneo la Kimondo Kwa ajili ya Maendeleo ya Kitalii na kiuchumi.

Ili kufikia Adhma hiyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo meiagiza Menejimenti ya Ngorongoro kuhakikisha inatenga Bajeti na kuwalipa Fidia Wananchi walio chukuliwa Eneo la Kimondo kabla ya uendelezaji wa eneo la kitalii.

Katika hilo Menejimenti ya Ngorongoro imemhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa kuwa mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga Bajeti kwaajili ya kulipa fidia Wananchi waliopo karibu na eneo la kimondo katika kijiji cha Ndolezi kata ya Mlangali Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.  

– Advertisement

By Jamhuri