Na Theophilida Feliciani, JamhuriMedia, Kagera

Ikiwa leo tarehe 29, Oktoba 2025 ni siku muhimu kwa Watanzania kuwachagua viongozi Mkuu wa Mkoa Kagera Hajath Fatma Mwassa ameungana na watanzania wengine kutimiza haki yake ya kuwachagua viongozi wa udiwani, wabunge na Rais.

Mkuu wa mkoa Mwassa ambaye amepiga kura kituo cha airiport ya zamani kata Miembeni Manispaa ya Bukoba akizungumza na waandishi wa habari eneo la kituo hicho amesema hali ya usalama ni tuvulu tangu kufunguliwa kwa vituo maeneo yote na wananchi wanaendelea kujitokeza na kupiga kura.

Amesema kuwa amezunguka maeneo mbalimbali ya wilaya za mkoa huo lengo ikiwa ni kuhakikisha amani na utulivu vinatawala muda wote ili zoezi hilo liweze kukamilika salama.

Hata hivyo amewasihi wananchi wote wenye sifa kujitokeza nakupigia kura ili kuwachagua viongozi watakaowatumikia kipindi kingine cha miaka mitano huku akiwahakikishia usalama umeimarishwa vya kutosha.

Wakati huo huo mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima amepiga kura yake kituo hichohicho ya airport ya zamani naye amesema wilaya ya Bukoba hali ni tulivu halmashauri zote mbili za Bukoba Manispaa na Bukoba Dc na wananchi wanaendelea kufika kwenye vituo na kutimiza wajibu wao wakupiga kura.