Baada ya ubishi na headlines za muda mrefu kuhusiana na mchezo wa El Clasico kati ya FC Barcelona dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa Camp Nou ni timu gani itaibuka mbabe dhidi ya mwenzake, hatimae usiku wa May 6 2018 macho na masikio ya mashabiki wa soka yalielekezwa Camp Nou.

FC Barcelona wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya Real Madrid magoli ya Barcelona yakifungwa na Luis Suarez dakika ya 10 na Lionel Messi dakika ya 52 wakati magoli ya Real Madrid wao yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 15 na Gareth Bale dakika ya 72.

Game hiyo ilimalizika kwa staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kucheza kwa dakika 45 pekee kufuatia kuumia enka jeraha ambalo litamuweka nje ya uwanja kwa wiki mbili lakini kikubwa amefikia rekodi ya mkongwe wa Real Madrid Destafano ya kuwa mchezaji wa Real Madrid aliyefunga magoli mengi kwenye El Clasico akifunga magoli 18 katika game 33 wakati De Stefano alifanya hivyo akicheza game 30.

 

Please follow and like us:
Pin Share