Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Simanjiro
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Ina mpango mkubwa ni kuhakikisha inafikisha huduma ya Maji kwenye Makao Makuu ya Vijiji vyote Wilayani humo.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Simanjiro Mhandisi Boniface Mushi alipokua akizungumza kwenye Mkutano wa nusu Mwaka na Viongozi wa vyombo vya Watumia Maji ulioandaliwa na RUWASA Wilaya na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwaheshimiwa Madiwani.
Mhandisi Mushi amesema RUWASA imejiwekea Mpango wake wa kuhakikisha huduma ya Maji inafika katika kila Makao Makuu ya kila Kijiji ili kusogeza huduma hiyo karibu na jamii hasa ukizingatia makazi ya jamii ya Wamasai wanaishi mbalimbali.
” Kama inavyofahamika jamii zetu za Wamasai makazi yao yako mbali mbali kidogo, unakuta kutoka kitongoji hadi kitongoji viko umbali mrefu , kwahiyo tutakapokuwa tumemaliza zoezi kuhakikisha Vijiji vyote vimepata huduma ya Maji , ndipo tutahamia katika hatua nyingine ya kwenye Vitongoji ” amefafanua Mhandisi Mushi.
Aidha amesema Kwa Sasa kazi inayoendelea ni Utekelezaji wa kuhakikisha Vijiji visivyokua na huduma ya Maji vinakua na maji kupitia visima 900 ambavyo vinachimbwa Tanzania nzima, ambapo kwa Wilaya ya Simanjiro wamepatiwa vitano (5) ambavyo Utekelezaji wake unaendelea mashine ziko Mahali husika ( Site)
Hata hivyo amesema RUWASA ina Mpango wa kujenga mradi ( Point source) ambao wananchi watakua wakipata huduma ya Maji katika eneo la chanzo.
Awali akielezea lengo la Mkutano huo Mhandisi Mushi amesema ni kuwakutanisha viongozi wa vyombo vya Watumia Maji akiwemo Mwenyekiti, Katibu na Mhasibu ili kibadilishana uzoefu katika shughuli zao za kiutendaji.
” Katika Mkutano huu pia wenye Viti wa vyombo vya Watumia Maji wameweza kuwasilisha taarifa zao mbele ya mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Jacob Kimeso aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Fakii Raphael Lulandala, lengo likiwa ni kutoa taarifa hizo ili kuona walikotoka, walipo sasa na huduma ya Maji inakoelekea” amesema Mhandisi Mushi.
Mwenyekiti wa Watumia Maji Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Zakayo Paulo amesema RUWASA imewasaidia kuwakutanisha pamoja na kuwapatia muongozo ambao umewabadilisha katika mitazamo ya kazi pamoja na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma juu ya uwajibikaji wao.
” Tunamshukuru sana RUWASA Wilaya ya Simanjiro, imekua ni msaada mkubwa kwani awali wananchi walikua wakipata huduma ya Maji Kwa kutembea umbali wa zaidi ya km.16 , hususani katika kitongoji Cha Katikati ambacho ndio kijijichenye shida kubwa ya Maji, ambapo RUWASA wameahidi kwenda kuchimbwa kisima kimoja cha maji.