Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Dodoma
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewasisitiza Watanzania kuwa kila mmoja awe mlinzi wa amani.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesema Rais Samia amehimiza kuendelea kufanya kampenzi za kistaarabu zinazozingatia utu wa Mwanza.
Kihongosi wamewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma leo Oktoba 5, kuwa amani ndiyo tunu ya Watanzania hivyo wanapaswa kuilinda.
Wito wetu wa mgombea urais, Rais Samia Suluhu Hassa ni kuendelea kufanya kampeni za kistaarabu zinazozingatia utu wa Mtanzania. Wito zaidi ni kwa kila Mtanzania kuwa mlinzi wa amani ya nchi, kwani amani na utulivu ndiyo tunu yetu Watanzania.

Kipindi hiki cha lala salama, CCM tumejipanga hakikisha tunamfikia kila Mtanzania na kumhamasisha apige kura Oktoba 29,ameema.
Amesema tangu mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia azindue kampeni zake Agosti 28, mwaka huu zaidi Watanzania milioni 45 wamefuatilia mikutano hiyo.
Amesema kati hao, milioni 14.6 wameshiriki kuhudhuria mikutana na milioni 31.6 wamefuatilia kwa njia ya mitandano mbalimbami ya kijamii.
Amesema hadi sasa Rais Samia amefanya mikutano 77 katika mikoa 21 katika kanda za Kati,Magharibi, Pwani, Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Pemba na Kanda ya Kaskazini.
Katika maeneo yote aliyofanya kampeni mgombea wetu Watanzania wameonyesha kuwa naye imani kubwa, wanajitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza katika kunadi ilani ya uchaguzi ya mwaka 2025-30.
Sera na ahadi zake zimeonyesha wazi kukubalika kwa sababu zimeendelea kubeba matumaini makubwa na matarajio ya Watanzania,amesema.

Akisisitiza juu ya imani hiyo, Kihongosi amesema si bahati wala mkubwa, bali imechagizwa na uongozi wenye mafanikio makubwa katika miaka minne aliyoshika madaraka.
Amesema imani ya wananchi kwa Rais Samia siyo ya bahati wala mkumbo, bali ni imechagizwa na uongozi wenye wa mafanikio.
Aliupokea mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerer (INHPP), ukiwa asilimia 37 hadi kufikisha asilimia 99.55, reli kuanzia reli ya Standard Gauge (SGR) kutoka Dar es Salaa, mpaka Makutupora kilomita 722, usafiri wa treni kati ya Dar es Salaam na Dodoma, vichwa vya reli 17 na mabehewa.
Wananchi wanajionea kazi ya ujenzi wa miundombinu kutoka Makutupora kwend Tabora hadi Isaka, kisha Isaka-Mwanza-Tabora kwenda Kigoma, Uvinza hadi Musongati ncgini Burundi, amejenga kilomita 15,366.36 ndani ya miaka minne.
Chini ya uongozi wake ndege sita 6 mpya zimenunuliwa hivyo kufanywa Shirika la Ndege Tanzania kuwa na ndege 16,amesema.
Amesema wananchi hasa wa vijijini wamekuwa mashuhuda wa kazi kubwa iliyofanywa ndani ya miaka minne,miradi 1,633 ya usambazaji wa maji imekamilika. Kati ya hiyo 1,335 ni ya vijijini pekee yake.
Sekta ya afya vituo vipya 1,368 vimejengwa, hospitalli zinazotoa huduma za dharura (EMD) zilikuwa saba, sasa zipo 116, vituo vyenye kutoa huduma za uzazi ukiwamo upasuaji vimejengwa.
Kwa upande wa sekta ya elimu, shule za msingi zimeongezeka hadi kufikia 19,783 kutoka 16,656, wakati Rais Samia anaingia madarakni shule za sekondari zimefikia 5,926, kutoka 5,001.
Amesema bajeti ya mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kutoka Sh bilioni 464 hadi 786, huku uchumi wan chi ukikuwa kutoka asimilia 3.9 hadi asilimi 5.5 mwaka 2024, wakati matarajio ni kufika asilimia 6, huku ajira milioni 8 zikitengenezwa ndani ya miaka minne.
Amesema utu ni falsafa ya Rais ambayo alianza kuitekeleza kwa kuwapa nyongeza mishara na kupandisha madaraja wafanyakazi, wakati huo wakiwa wamesimama bila kuongezewa kwa muda wa miaka saba.
Wananchi wanajitokeza kwa sababu hayo ni baadhi ya mambo ambayo yanagusa maisha ya Watanzania, kuna marufuku ya kuzuia maiti kwa sababu ya bili za matibabu, bima ya afya kwa wazee,watoto na walemavu, wagonjwa wa saratani, sukari na figo kutibiwa bure, kuanzisha mchakato wa Katiba mpya ndani ya siku 100, kutoa Sh bilioni 200 kwa wafanyabiashar wadogo, ajira mpya za walimu na wahudumu wa afya, haya yote yatafanywa na Rais Samia,amesema.

Amesema kuanzia Oktoba 7, Rais Samia ataanza ziara zake kampeni katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Mwanza,Shnyanga, Mara, Kagera, Geita na Kagera.
Matarajio yetu ni kwamba mikutano itaendelea kufanya vizuri kwa sababu ya mafanioko yakiwamo daraja la Busisi kukamilika, chanzo cha maji butimba kinachonufaisha wananchi 450,000 Mwanza, mradi wa Ziwa Victoria unahudumia wananchi 86,980 wa Tinde na Shelui, ujenzi wa vivuko sita Ziwa Victoria umekamilika, boti ya kuhudumia majeruhi wa ajali (Ambulance), chanjo za mifugo imezinduliwa na Sh bilioni 62 zimetolewa.