Na Kulwa Karedia, Jamhuri Media-Tanga

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema amejipanga kuongeza upanuzi wa Bandari ya Tanga ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa reili ya kisasa kutoka Tanga-Arsuha mpaka Musoma yenye urefu wa kilomita 1,108.


Samia ametoa ahadi hiyo wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Tanga na vitongozi vyake wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu Septemba 29,2025.


Tutaanza utekelezaji wa mradi wa reli itakayounganisha Bandari ya Tanga kuelekea Arusha mpaka Musoma yenye urefu wa kilomita 1,108, reli hii itafunguwa maeneo ya viwanda na kuongeza fursa za ajira ndani ya mkoa huu.


Pamoja na hayo, tumeunganisha na maeneo mengine, watakaojenga reli hii ni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), watasaidiana kujenga bandari na barabara zinazounganisha maeneo haya hasa babarabara ya Handeni,amesema
Bandari ya Tanga inakwenda na uamuzi tulioufanya ya kuwa mji eneo hili ndilo bohari ya mafuta na gesi, hili litachangia kuzalisha ajira mpya nyingi 2109, hili linakwenda kunyanyua uchumi wa wana Tanga.


Mbali ya mradi huu kama manavyojua tuna mradi mwingine wa mkakati unafungamana na bandari hii, moja wapo ni mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka hapa Tanga, mradi huu umekamilika kwa asilimia 84 na umeleta manufaa mengi wakimo watu 1,300 wameajiriwa na ndani ya Wilaya ya Tanga wameajiriwa watu 2,000,amesema.


Kuhusu miradi mingine, amesema ujenzi wa daraja la Mto Pangani na barabara ya Bagamoyo-Sadani hadi Tanga, nataka kuwambia nimetoka Pangani leo, nimeona maendeleo mazuri ya kazi hii, ujenzi Tanga-Panga kilomita 50 imefikia asilimia 75.


Ujenzi wa barabara ya Sadani-Mavuruke kilimota 55 ujenzi wake umefikia asilimia 50 na ujenzi wa daraja la mto Pangani la mita 525 limefikia asilimia 62. Ahadi yetu wana Tanga ni kukamilisha miradi yote inayounganisha mikoa ya Tanga na Pwani itakayochangia kubadilisha uchumi wa ukanda wa pwani,amesema.


amesema barabara hiyo itasaidia kupunguza masafa kwa kilomita 100 kwenda Bagamoyo na kuingia Dar es Salaam.


Tutafanya upanuzi na ukarabati mkubwa kwa barabara ya Tanga-Segera-Chalinze mpaka Dar es Salaam yemye urefu kilomita 686, tunazipanua kwa sababu ya kupunguza msongamano mkubwa magari,amesema
Amesema mwelekeo wa serikali ni kuirejesha Tanga ya viwanda kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kujenga Tanzania ya viwanda kwa kuanzisha na kutengeneza kongoni za viwanda kila wilaya.


Tumejipanga kufufua viwanda vilivyoanzishwa na kuendeleza kikiwamo kiwanda cha chai Korogwe, pia nimefurahi kuona kiwanda kipya kufunga magari ya ambulance kinakuja kujengwa hapa, tutaendelea kuvuta wawekezaji zaidi.


Kutokana na hali hiyo, amewaomba wananchi wa mkoa huo ambao maeneo yao hayatumiki lakini yako mikononi mwa watu wafanye hima yarudishwe kwa ajili ya wawekezaji wanaokuja wakute yako tayari.


“Ili kukuza ajira za vijana, serikali imekuja na Mpango Jenga Kesho iliyobora (BBT) ambayo inajihusisha na maeneo ya uvuvi, kilimo na madini, hapa kwenu tunakuja eneo la kilimo na madini,amesema.


Kuhusu sekta ya madini wameanzisha maeneo ya wachimbaji wadogo waweze kuchimba ili waendeleze uchumi wao.
Hapa Tanga tumetoa leseni kwenye maeneo mbalimbali na upatikanaji wa dhahabu umeendelea vizuri, tutaendelea kuweka nguvu kupata maeneo mengine vijana waingie kwenye uchimbaji ili kuboresha maisha yao,amesema.


Kuhusu kilimo amesema ataanzisha mashamba makubwa ya umwagiliaji maji kwa ajili ya vijana. Amesisitiza Pangani kuna mradi mkubwa wa Bonde la Pangani ambako serikali inakwenda skimu kubwa ya umwagiliaji ambayo itasaidia kutunza shamba kubwa na kujenga kiwanda cha sukari ambacho kitazalisha sukari ya brown. Kiwanda kingine kitajengwa bandarini Tanga kwa ajili ya kuzalisha sukari ya viwanda.


Katika bonde la Pangani amesema wananchi 20,000 watafaidika na kilimo cha umwagiliaji kwa msimu wote wa mwaka mzima
Kwa upande wa masoko, amesema watajenga soko la kisasa ili wafanyabisha wadogo maarufu Wamachinga 1,400 wataweza kulitumia kwa Sh bilioni 1.7
Amesema ili kuwajengea uwezo wavuvi, serikali itajenga soko la samaki la kimataifa ambalo litaondoa kero zilizopo.


Amsema kipindi kilichopita walitoa boti 15 kuvua samaki masafa marefu sambamba na vifaa ambavyo vimesaidia shughuli hizo kutenda vema.


Kwenye sekta ya afya, amesema wamekeza ujenzi wa hospitali kila wilaya ili kusogeza huduma karibu, wamejenga vituo vya afya na zahanati nyingi.


Kama mtatupa ridhaa sasa tunakwenda viwanda vya vifaa tiba nchini pamoja, bima ya afya ndani ya simu 100 za uongozi wake tutaanza majaribio kwa watu weote
Kuhusu migogogro ya ardhi atahakikisha wanaipunguza kwa kiasi kikubwa kuendelea kupima maeneo.