Na Mwandishi Jamhuri Media, Kigoma

Mgombea bunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba, ametoa wito kwa wananchi wa Kigoma kumchagua mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan.

Amesema hatua hiyo inatokana na kumpa kura Rais Samia kupeleka maendeleo makubwa mkoani humo katika kipindi cha uongozi wake wa miaka minne.

Amesema mkoa huo umenufaika na bajeti ya maendeleo ya Sh trilioni 11.4, ambayo ni ishara ya upendeleo wa kwa mkoa huo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja wa Katosho leo Septemba 14, 20205, Serukamba amesema Serikali ya imefanya kazi kubwa ya kuifungua mkoa kiuchumi.

Amesema Serukamba shughuli za bandari zimeongezeka kwa kiwango kikubwa, kutoka tani 18,000 hadi tani milioni 32, jambo linalothibitisha dhamira ya dhati ya serikali kuimarisha sekta ya usafirishaji na biashara.

Amesema sekta ya elimu, Rais Samia amejitahidi kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto kwa kuongeza miundombinu na rasilimali.

Amesema Rais Samia ameanzisha mradi mkubwa wa kuunda Gridi ya Taifa ya Maji ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama.

Amesema jambo hilo litaondoa changamoto ya uhaba wa maji katika maeneo mengi ya nchi.

Amesema mkoa huo sasa imenufaika na bajeti ya maendeleo ya Sh trilioni 11.4, ambayo ni dalili ya upendeleo wa wazi kwa mkoa huo.

amesema Rais Samia amejenga hospitali kila halmashauri na vituo vya afya 28, sambamba na ujenzi wa Hospitali ya Kanda.

Amesema Ziwa Tanganyika, Serikali inajenga meli tatu mpya, huku pia kukiendelea ujenzi wa uwanja wa ndege na miundombinu mingine ya kufungua mkoa huo kupitia usafiri wa maji.

Kuhusu nishati, Serukamba alisema kati ya vijiji 239 vilivyokuwepo Kigoma, vyote vimepata umeme isipokuwa baadhi ya vitongoji ambavyo viko kwenye mpango wa kumaliziwa kupitia ilani ya uchaguzi.