Waokoaji katika ukanda wa Gaza wamesema mashambulizi ya Israel yaliyofanywa leo Jumatano yamewaua watu 29 na wengine wamejeruhiwa katika eneo la kaskazini mwa Gaza la Jabalia.
Waokoaji katika ukanda wa Gaza wamesema mashambulizi ya Israel yaliyofanywa leo Jumatano yamewaua watu 29 na wengine wamejeruhiwa katika eneo la kaskazini mwa Gaza la Jabalia.
Mashambulizi hayo yamefanyika wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipokuwa na mazungumzo na mjumbe wa Marekani Steve Witkoff kuhusu kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas.
Mapema wiki hii kundi la wanamgambo wa Hamas lilimuachilia mateka mmoja mwenye uraia wa Marekani na Israel, Edan Alexander na baada ya hapo Israel imeanzisha tena mashambulizi ambayo mpaka sasa yamewauwa zaidi ya watu 70 katika muda wa saa 24.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kwamba wanajeshi wa Israel wataendelea kuishambulia Gaza licha ya juhudi zinazoendelea za kusitisha mapigano.