Kikosi cha Taifa Stars, kimelazimishwa sare ya bila kufungana kikiwa ugenini dhidi ya wenyeji wake Uganda.
Mechi hiyo ya kuwania kufuzu Afcon imepigwa kwenye Uwanja wa Namboole jijini Kampala na Stars iliyokuwa ikiongozwa na nahodha Mbwana Samatta imeonyesha soka safi na kuwapa wakati mgumu Uganda.
Stars ilifanya mashambulizi mengi zaidi langoni mwa Uganda, hasa katika kipindi cha pili, hali iliyowalazimisha walinzi wa Uganda kufanya faulo nyingi zaidi.
Kipindi cha kwanza ilionekana Uganda wakiwa na nafasi nyingi ambazo hawakuzitumia huku mvua kubwa iliyonyesha dakika chache kabla ya mechi ikiwa imechangia kuvurugika kwa uwanja huo.
Hata hivyo, kipindi cha pili, Waganda walishambulia kiasi huku Stars kupitia Samatta, Thomas Ulimwengu na Saimon Msuva wakionyesha kiwango cha juu. Nafasi kadhaa nao walishindwa kuzitumia.
Mabeki kam Abdi Banda, Aggrey Morris, Hassan Kessy, David Mwantika, Gadiel Michael wakishirikiana na viungo Frank Domayo, Mudathir Yahaya na Himid Mao aliyeingia baadaye wakioneysha soka la kiwango cha juu.
Stars inayonolewa na Kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike, imefikisha pointi 2 katika Kundi L linaloongozwa na Waganda wenye pointi.
Please follow and like us:
Pin Share