Jeshi la Sudan Kusini limeamuru raia wote pamoja na wafanyakazi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na wahudumu wote wa mashirika ya msaada kuondoka katika kaunti tatu za Jimbo la Jonglei, kabla ya operesheni ya kijeshi.
Jeshi la Sudan Kusini limeamuru raia wote pamoja na wafanyakazi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na wahudumu wote wa mashirika ya msaada kuondoka katika kaunti tatu za Jimbo la Jonglei, kabla ya operesheni ya kijeshi dhidi ya vikosi vya upinzani. Katika taarifa yake, jeshi limewataka raia wote wanaoishi katika kaunti za Nyirol, Uror, na Akobo katika Jimbo la Jonglei kuondoka mara moja kwa usalama na kuelekea katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali haraka iwezekanavyo.
Taifa hilo changa barani Afrika, limekumbwa na mapigano kwa miezi kadhaahuku Umoja wa Mataifa ukisema mapigano hayo yanafanyika kwa kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu mwaka 2017.
Mapigano makali yameripotiwa katika jimbo la Jonglei, ambako Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) linapambana na wapiganaji wanaoiunga mkono Jeshi la Ukombozi la Sudan – Upinzani (SPLA-IO).


