Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Manyara

Mratibu wa Kampeni Kanda ya Kaskazini na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mvumilivu mno.


Sumaye ametoa kauli hiyo wakati akisalimia maelfu ya wananchi wa Manyara wakati wa mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa zamani wa mabasi mjini Babati mkoani Manyara leo Oktoba 4,2025.


Amesema Rais Samia ni kiongozi mwenye upeo wa mbali mno uliombatana na uvumilivu kutokana na kurushiwa maneno mengi na watu wasiomtakia mema.


“Katika miaka minne umevumilia mengi mama, tuaamini uvumilivu huu ni kwa sababu unawapenda Watanzania.
“Unasemwa mambo mengi, umeendelea kuvumilia.
“Anayepigwa vita siyo Samia, wanaopiga vita, wanatamani CCM ianguke.
“Kinachofafutwa ni CCM kuanguka, sasa wanahamia kwa mgombea wetu,
Sisi Watanzania tutawajibu kamwe CCM haikiangushwi kirahisi,”amesema.


Amesema Rais atafanya kazi kubwa ndani ya miaka mitano ijayo kama atashinda na atawanyamazisha wote wanaompinga.
“CCM na mgombea wetu wakiingia madarakani ndani ya miaka ijayo itawanyamazisha wote,”amesema.


Kuhusu uchapaji kazi, Sumaye amesema Rais Samia amefanya vizuri ndani ya miaka minne na ndiyo maana akaweka mpango wa dira ya Taifa ya miaka 25 ili hata viongozi watakaokuja wazidi kunyosha atakapoishia.


“Rais Samia hakuangalia miaka minne tu, akiamua kutengeneza Dira ya Maendeleo ya Taifa kwa miaka 25, yeye hatakuwepo, lakini anataka kuona Tanzania ilipo na itakapokuwa miaka hiyo.


“Katika miaka mitano ameomba kuonyoosha barabara hii ya miaka 25 ili ang’oe visiki na kunifika mabindo ili watakaokuja wazidi kuendeleza hapo.


Amesema tangu yeye na wenzake wateuliwe kuwa waratibu wa kampeni, wamefanya kazi nzuri ambayo itakipa ushindi chama hicho.
“Tunakushuru sana kwa kututeua kuwa waratibu, tumefanya kazi nzuri, tumeshirikiana na waratibu na Kamati za siasa za wilaya na mikoa.


“Tumefanya kazi yetu vizuri tunaamini mambo yatakuwa safi, kama kuna upungufu tusamehe.


“Ziara yako imetupa nguvu mpya, chaji, ukiondoka ndiyo tunaanza upya kabisa, watu Hawa wamesema watakupa kura asilimia 90, nataka kukuhakikishia wamesema watakupa kura asilimia 90.


“Tunasema ikishuka walau ibaki asilimia 85, ishuka hapo usituchape viboko.
Amesema Samia amewapa nguvu mpya na hata atakapoondoka wataanza kazi tena ya kupita maeneo mbalimbali.


” Watu wameonyesha wanakupenda,popote
tulipopita watu wanasema kula zako hazina shaka.