MWILI wa Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Richard Tamilway maarufu kwa jina la ‘Tambwe’ aliyefariki dunia juzi asubuhi nyumbani kwake Mbagala Kizuiani, unatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi katika Makaburi ya Temeke Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu aitwaye Charles Tamilway amesema kuwa taratibu za kuuhifadhi mwili wa kaka yake katika nyumba yake ya milele zipo zimekamilika mwili huo utahifadhiwa leo Jumamosi mchana katika makaburi ya Chang’ombe maduka mawili, Dar es Salaam.
Naye mjane wa marehemu, Mariamu Masoud, alisema mume wake hakubahatika hata kufika hospitali kupata matibabu ya kuokoa maisha yake baada ya kuugua ghafla, hivyo anamuomba mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mumewe mahali pema peponi.

Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa Chama cha Wananchi (CUF), baadaye akahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa chama hicho na mwaka 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA.

Please follow and like us:
Pin Share