Na Francisco Peter, Dar es Salaam

Tanzania ni miongoni nchi zinazofanya vema katika utekelezaji mifumo ya matumizi TEHAMA kwenye sekta ya afya.

Tayari ipo mifumo kuanzia ngazi kata ambapo imeweza kukusanya taarifa ngazi za chini kwenda hadi kitaifa ambayo usaidia serikali kwenda kufanya maamuzi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi TEHAMA Wizara ya Afya Silvanus Ilomo katika Mkutano wa 12 wa Afya Tanzania (THS) unaofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

“Hatua hiyo ya kukusanya taarifa inasaidia serikali kuweza kufanya maamuzi ikiwemo kujenga vituo vya Alafya, kusaidia kufikiwa kwa usambazaji wa dawa kwa pamoja,” amesema Ilomo.

Ilomo anasema juhudi hizo zinaongeza tija ilikubadilisha utoaji wa huduma za afya na kusogeza karibu upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote na
kufikiwa kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa figo na presha pamoja na mengineyo.

Aliongeza kusema kuwa hali hiyo ya kupata takwimu ujumuishi imeonekana kusaidia sana eneo la utakii tiba idadi kubwa sasa ya utalii tiba; idadi ya watalii wamekuwa wakifika kupata utalii wa aina hiyo.

Aidha amesema kuwa mfano wa hospitali kama za JKCI na MOI na nyinginezo zimekuwa zikipokea kwa wingi wagonjwa wanaotoka nje ya nchi kwaajili ya kupata matibabu.

Tanzania tumekuwa tunafanya vizuri katika eneo la teknilojia katika afya (Global Immaturity Assessment) katika nchini zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Wakati huo huo, Taasisi ya Kisuez iitwayo SOLIDARMED inayofanya kazi katika Mkoa wa Morogoro chini ya Mkurugenzi wake Benarus Sambili wameweka banda katika Mkutano huo wa 12 wa Afya Tanzania (THS).

“Tumeweza kuweka banda letu katika mkutano huu, tumekuwa tukifanya kazi na Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI,” amesema Sambili.

Sambili amesema katika kufikisha huduma tumeweza kuwa tunawafikia makundi ya wafugaji waliopo wilayani Malinyi mkoani Morogoro .

Amesema wamekuwa wanawafikia kaya za wafugaji na kwa watu wengine , kaya za wafugaji maranyingi zimekuwa hazikai pamoja hivyo imekuwa kupata kwao huduma za afya ni ngumu .

” Katika Mkutano wa huu wa 12 wa Afya Tanzania (THS) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam wamefika hapo kushiriki kuonesha kazi tunafanya na pia tunajifunza kutoka kwa wenzetu na tunaenda kuboresha huduma za afya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe tayari alifungua maonesho hayo ambao amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, sasa tuna mfumo jumuishi wa rekodi za matibabu za kielektroniki unaounganisha taarifa za mgonjwa kuanzia ngazi ya jamii, vituo vya afya, hospitali za wilaya mpaka taifa,.

Dkt. Shekalaghe.amesema serikali inajivunia mfumo wa kidigitali wa M-Mama ambao unaratibu usafiri wa dharura kwa mama wajawazito na watoto wachanga walioko kwenye hatari, kupitia namba 155 bila malipo.

“Kama mfumo rasmi wa kitaifa wa usafiri wa dharura wa kina mama, M-mama sasa unahudumia mikoa yote ya Tanzania na unatarajiwa kusafirisha wanawake na watoto wachanga 50,000 kila mwaka kupata huduma wanazohitaji.

Aidha Dkt. Shekalaghe amewahimiza washirika na wadau wote waliohudhuria katika mkutano huo kuendelea kuunga mkono kwani mkutano huo si mkutano wa kila mwaka tu bali umekuwa jukwaa kuu la afya nchini Tanzania mahali pa mawazo, ushirikiano, na uwajibikaji.