Kwa mara ya kwanza Tanzania imeadhimisha miaka 51 tangu kuvumbuliwa kwa madini ya kipekee ulimwenguni, Tanzanite.

Maadhimisho hayo yalidogoshwa kutokana na Taifa la Tanzania kuwa katika maombolezo kwa siku tatu mfululizo kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere Alhamisi wiki iliyopita , kilichozama katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza.

Madini haya husherehekewa ulimwenguni na mashirika ,taasisi na wafanya biashara mbalimbali wa madini ulimwenguni lakini hayajawahi kusherehekewa ama kuadhimiwa hata siku moja nchini Tanzania , Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation , imeona iadhimishe siku hii kwa kutoa taarifa na kuudhihirishia ulimwengu kuwa, madini ya Tanzanite ni fahari na urithi wetu Watanzania.

Maadhimisho hayo yalipangwa kufanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yakihudhuriwa na mgunduzi wa madini hayo, Jumanne Mhero Ngoma.Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Asha Mhero Ngoma amesema waliandaa sherehe kubwa lakini kutokana na msiba wa kitaifa uliopo wameona wazungumze na waandishi wa habari tu.

Tanzanite Founder Foundation ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali , iliyoanzishwa na kusajiliwa mwaka 2013 , ikiwa na lengo kuu la kuwajengea uwezo vijana na watu wote waishio maeneo yote yanyozunguuka migodi na maeneo ya jirani ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku kutokana na madini hayo .

Tanzanite Founder Foundation Jumapili hii imeona iadhimishe miaka 51 ya madini ya Tanzanite tangu madini haya ya kipekee duniani kuvumbuliwa kw amara ya kwanza nchini Tanzania.

Madini haya husherehekewa ulimwenguni na mashirika ,taasisi na wafanya biashara mbalimbali wa madini ulimwenguni lakini hayajawahi kusherehekewa ama kuadhimiwa hata siku moja nchini Tanzania , Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation , imeona iadhimishe siku hii kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na madini hayo ikiwa ni pamoja na kutoa historia fupi ili kutoa tathmini ya tulikotoka , tulipo kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuudhihirishia ulimwengu kuwa, madini ni fahari yetu na urithi wetu Watanzania.

Asha alisema huu ni wakati sahihi wa kuitangazia dunia kuwa madini ya kipekee ulimwenguni Tanzanite yanapatikana Tanzania badala ya kuacha nafasi hiyo kwa baadhi ya mataifa ambayo hufanya sherehe za kujiongezea soko kwa kuyatangaza kuwa yanatoka katika nchi zao.

“Kenya, India na China ndiyo wauzaji wakuu wa Tanzanite katika masoko makubwa ambayo ni Marekani na Bara la Asia lakini ukweli ni kwamba huo ni urithi wetu Watanzania. Tusiposema sisi watasema wao na watatunyang’anya asili yetu,” alisema Asha.

Kuhusu manufaa ya madini hayo na hatua zinazochukuliwa na Serikali kuyalinda, Asha alisema ujenzi wa ukuta ni hatua muhimu ya kuyatambua madini hayo na kuhakikisha thamani yake inalindwa.

Asha alisema taasisi hiyo mwezi ujao inatarajia kufanya mkutano mkubwa wa wadau wa Tanzanite kujadili namna madini hayo yanavyoweza kuleta manufaa zaidi kwa Taifa la Tanzania.

Mgunduzi wa madini hayo, Mzee Ngoma alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutambua mchango wake na kumpa fedha za matibabu na kusisitiza yeyote anayetaka kujua kuhusu uvumbuzi wa madini hayo

amtafute.

Please follow and like us:
Pin Share