Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulika na Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado ameongoza ujumbe wa kutoka Nchini Tanzania kupeleka misaada ya unga, mahindi, mablanketi, mahema na dawa mbalimbali ambazo zitasaidia wahanga wa Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kyela Bwn. Godfrey Kawacha akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Karonga Nchini Malawi Roderick Mateauma (Kulia) kabla ya Magari yaliobeba Misaada ya Kibinadamu ya kuvuka Mpaka wa Kasumulu kuelekea Mjini Blantyre Malawi.

Luteni Kanali Masalamado amesema hayo wakati Msafara wa magari ya jeshi la Wanachi wa Tanzania yakivuka mpaka wa Kasumulu wilaya ya Kyela kuelekea Mji wa Blantyre Nchini Malawi tarehe 22/03/2023.

“Natoa pole kwa ndugu zetu, wananchi wa Malawi tuko nao katika hali hii ngumu,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.

“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,” amesema

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado  (katikati) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Karonga Nchini Malawi Roderick Mateauma.  

“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Karonga Nchini Malawi Roderick Mateauma ameishukuru Serikali na kusema kwamba msaada huo utasaidia kupunguza athari kwa wahanga na inaonesha mahusiano ya karibu yalipo kati ya nchi hizo mbili.

Magari ya Jeshi la wananchi Tanzania yaliyobeba vifaa mbalimbali vya msaada wa kibinadamu yakivuka mpaka kuelekea mjini Blantrey.

By Jamhuri