đź“ŤBERNE, USWISđź“Ť
Tanzania imeibuka kidedea katika uchaguzi wa mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Ubora wa Huduma wa Umoja wa Posta Duniani katika uchaguzi uliofanyika leo tarehe 21 Februari, 2025 Makao Makuu ya Umoja wa Posta Duniani (UPU) jijini Berne, Uswis.
Â
Katika uchaguzi huo, mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Clarence Kuberwa Ichwekeleza, ambaye ni Mkurugenzi Uendeshaji wa Shirika la Posta Tanzania aliibuka mshindi baada ya kupata kura 30 dhidi ya mpinzani wake kutokea nchi ya Cameroon aliyepata kura 14.

Â
Kwa ushindi huu, Mhandisi Clarence atashiriki kwenye vikao vya Bodi hiyo ya maamuzi ambayo inahusika na kupitisha fedha kwa ajili ya miradi ya kuboresha huduma za Posta kwa nchi zote wanachama wa UPU ikiwemo Tanzania. Tanzania itanufaika na uwepo wa Mhandisi Clarence kwenye vikao vya maamuzi ya miradi itakayoombewa fedha kwenye Mfuko huo.
Bodi ya Mfuko wa Ubora wa Huduma (QSF – Board) ina jukumu la kusimamia Mfuko katika kuidhinisha na kusimamia utekelezaji wa miradi iliyoidhinishwa kwa nchi wanachama wa Umoja katika kuboresha huduma za posta.
Â
Mfuko huu ni jukwaa la ufadhili kwa nchi wanachama kutekeleza miradi inayolenga kuboresha ubora wa huduma za mtandao wa Posta kimataifa pamoja na kuimarisha mtandao wa Posta ndani ya nchi. Mfuko unafadhili miradi inayogusa maslahi mapana ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ambapo mwaka 2024 pekee imefadhili miradi yenye thamani ya Dola za marekani17,009,241.

