Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,Jamhuri

Wakat leo ni siku ya Kifua Kikuu (TB) Duniani, Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 30 zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa ya ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Health Promotion Tanzania(HDT), Dk Peter Bujari, ambaye amesema nchi hizo 30 zenye maambukizi makubwa zinachangia kwa asilimia 87 ya maambukizi yote duniani.

Amesema kwa takwimu za mwaka 2023 Tanzania ilikuwa na wagonjwa wapatao 128,000 na kwamba hadi sasa maambukizi mapya ni 100,000 na wagonjwa 18,000 wamepoteza maisha sawa na kusema kila siku watu 50 hufariki kwa ugonjwa wa Kifua Kikuu hapa nchini.

“Tunapoadhimisha siku ya Kifua Kikuu duniani tukumbuke kuwa ni jukumu letu sote kuungana kwa pamoja kutokomeza ugonjwa huu,” amesema.

Amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa vikwazo vya kiuchumi na kijamii kunasababisha madhara makubwa yanayoambatana na kuongezeka kwa ugonjwa huo, ambao ni wa tisa duniani katika orodha ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi zaidi ya virusi vya Ukimwi.

“Bara la Afrika kila mwaka wagonjwa wa TB huongezeka kutokana na changamoto ya huduma za afya na rasilimali duni,mwaka 2022 watu milioni 2.5 waliugua TB Bara la Afrika ikiwa sawa na robo ya wagonjwa wote wapya wa TB duniani, ” amesema.

Bujari amesema ilikadiriwa watu 42,4,000 walikufa kutokana na ugonjwa wa TB Bara la Afrika mwaka huo hivyo asilimia 33 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa TB Duniani vinatokea Bara la Afrika.

Amezitaja nchi za Afrika zinazoongoza kwa TB ni Angola, Botswana, Cameroon, Congo, Somalia, Ethiopia, Cabon, Guinea Bissau, Guinea Sierra Leone , Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Namibia,Zambia ,Malawi na Liberia.

Please follow and like us:
Pin Share