Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Arusha umetimiza maagizo ya serikali kwa kuanza rasmi kutumia Mfumo mpya wa kidigitali wa Usimamizi wa kazi za matengenezo (MUM) ambao unatajwa kuwa suluhisho la kuondoa urasimu kwa wateja waliokuwa wakilazimika kufika moja kwa moja katika karakana kupata huduma.

Akizungumza katika kikao hicho kulichoshirikisha wadau wa maendeleo wa huduma za ufundi mkoani Arusha ,Mratibu wa mfumo wa MUM ,Mhandisi Pongeza Semakuwa amesema kuwa, huduma za Temesa zinakwenda kuwa bora kwa gharama nafuu na kumsaidia mteja kupata taarifa za matengenezo kwa haraka.

Mratibu wa mfumo wa MUM ,Mhandisi Pongeza Semakuwa akitoa elimu katika mafunzo hayo jijini Arusha

Amesema kuwa ,wanaendelea na zoezi lao la kutoa mafunzo kwa watumiaji wa mfumo huo ambapo mkoa wa Arusha ni mkoa wa 13 ambapo washiriki wa mafunzo hayo ni wateja wanaohudumiwa na Temesa watumishi wa Temesa wenyewe,karakana saidizi ,na watoa huduma za vipuri .

Amesema kuwa mfumo huo ni maagizo ya serikali kuhakikisha kuwa unaundwa na unatumika kwenye taasisi zote za serikali ukiwa umelenga faida kuu tatu ambazo ni kurahisisha utaratibu wa kupata huduma kutoka ofisi za Temesa nchi nzima ,kuhakikisha huduma za Temesa zinafanana kwenye kila kituo.kuanzia ubora na alama, ambapo nyingine ni kumsaidia mteja kupata taarifa za matengenezo akiwa amekaa kwenye dawati lake .

“Mapokeo ya mafunzo ni mazuri kwa kuzingatia maboresho yanayoendelea ndani ya taasisi mfumo huo ni.lazima na ni munimu sana .”amesema.

Meneja wa TEMESA Mkoa wa Arusha, Mhandisi Billy Munishi akionyesha baadhi ya teknolojia ya kisasa ambayo inatumika kutengeneza magari ofisini kwake .

Aidha ametoa rai kwa Taasisi wanazoshirikiana nazo ,gereji teule na wazabuni wawaunge katika kuutumia huo mfumo kwani kwa upande wao kama wakala wanajitahidi kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi vizuri.

Naye Meneja wa TEMESA mkoa wa Arusha , Mhandisi Billy Munishi amesema kuwa ,sasa hivi kuna mabadiliko makubwa yanayoendelea Temesa ambapo amesema
kubadilika sio tu kwenye kutumia mfumo hata kutumia vitendea kazi vya kisasa ili kuhakikisha mteja sasa hivi anatulipa fedha zake na anatulipa.kwa wakati ni vizuri kwani nao wanatengeneza na kulitoa kwa wakati na hiyo ndio Temesa ilivyo sasa hivi.

Munishi amesema kuwa, moja ya changamoto kubwa waliyokuwa nayo ni magari kukaa muda mrefu kwenye karakana kwani walikuwa wanachelewesha katika matengenezo na kuchukua muda mrefu ila kwa sasa wameboresha vifaa vya vitendea kazi na kuondokana na hiyo changamoto.

Amefafanua kuwa ,kwa sasa hivi badala ya kutumia masaa mawili wataweza kutumia lisaa limoja katika matengenezo hivyo kwa sasa hivi Temesa ni sehemu sahihi kwa watu kuleta magari yao ili waweze kuhudumiwa.

Ameongeza kuwa, mwanzo kwenye kufungua magari walikuwa wanatumia hata lisaa limoja lakini kwa sasa hivi ni dakika sita mpaka saba tayari unakuwa umeshamaliza zoezi zima la kufungua .

Kwetu sisi ni ufanisi mkubwa sana lakini kinachowasaidia ni vitendea kazi ambavyo ni bora kwa ajili ya kufanya hizo kazi na tayari vifaa vyote vinatumika na kila mtendakazi ana kifaa kizuri cha kufanyia kazi “amesema .

Ametaja changamoto waliyokuwa wanakabiliana nayo mwanzo kabla ya kuwa na vifaa vipya ni pamoja na muda wa kutengeneza magari ulikuwa ni mrefu ila kwa sasa hivi baada ya kuboresha vitendea kazi vya kisasa ule muda umepungua .

“Magari sasa hivi ukiangalia mwanzo tulikuwa tunatengeneza magari manne mpaka sita kwa siku ila kwa sasa hivi wanaenda hadi magari 20 kwa siku hivyo ukiangalia kwa namna hii hivi vitendea vya kisasa vimeenda kurahisisha utengenezaji wa magari .”amesema .Munishi.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo, Afisa usafirishaji kutoka TANROADS ,Amon Bashweka amesema kuwa,anamshukuru sana Rais Samia kwa kufanikisha huo mfumo ambao utawasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuweza kufanikiwa katika sekta hiyo ya usafirishaji na matengenezo ya vifaa vya taasisi kwa ujumla kwani mfumo huo.utawasaidia kuweza kuweka data na mifumo iliyosahihi na kwa urahisi zaidi na utasaidia pia kuweka ushawishi mkubwa katika Taasisi katika maswala mazima ya manunuzi

Mafunzo hayo ya Mfumo wa usimamizi wa matengenezo (MUM) ni ya 13 kwa mkoa wa Arusha ambayo yanafanyika nchi nzima.