Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA inasema mikoa ya Geita na Mara hali ya mawingu mvua katika machache ngurumo na vipindi vya jua.
Aidha taarifa hiyo imeeleza visiwa vya unguja na Pemba mikoa ya Tanga,Dar es Salaam Mkoa wa Pwani ikijumuisha na visiwa vya Mafia na Pemba hali ya mawingu machache ngurumo na vipindi vya jua.
Wakati huo huo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA katika taarifa yao hiyo wametoa angalizo la vipindi vifupi vya upepo mkali kilometa 40 kwa saa vinatazamiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani na Bahari ya Hindi mikoa ya Lindi,Mtwara,Dar es Salaam ,Tanga, ikijumuisha visiwa vya Mafia na Unguja na Pemba.
