Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mamla ya Mapato Tanzania (TRA), imetaja mbinu itakazotumia kuzuia upotevu wa mapato yatokanayo na biashara za mtandaoni ikiwemo kutumia wanunuzi pamoja na mawinga kuwapatia taarifa.
Hayo yalisemwa leo Agosti 9, 2025 na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda wakati wa semina ya uzinduzi wa Kampeni ya elimu ya kodi kwa biashara za mitandao iliyojumuisha, wawakilishi wa makampuni ya simu na benki wafanyabiashara biashara wa Mitandao,wahariri wa vyombo vya habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Baraza la Sanaa Nchini (BASATA).
Amesema hawana nia ya kuua biashara zao bali nikuwasaidia kuziendeleza ,hivyo wataendelea kuwahudumia wafanyabiashara vizuri ili waendelee kulipa kodi kwa hiari na kuweza kuongeza sifa ya kukopesheka.

“Niweke wazi kuwa tutatumia teknolojia kuwapata na zaidi tutatangaza dau kwa wanunuzi wapewe risiti na muuzaji huyo na kama hajapewa atoe taarifa TRA ili sisi tufuatilie na kulipwa na baada ya kulipwa asilimia tatu atapewa mnunuzi kwa sababu ndiye kasaidia kodi hii kupatikana,”amesema Mwenda
Ameongeza,”Hata kama wewe ni winga umeuza mzigo wa milioni moja tulipe laki moja yetu kwainutajivuniankuwa umechangia barabara unazopita, shule na hata hospitali alafu tupe maelekezo ya ule mzigo wa milioni ilitujue kama kodi stahiki imelipwa,”
Mwenda amesema katika mabadaliko ya sheria ya kodi ya mwaka 2025,TRA imesamehe VAT kwa wafanyabiashara wadogo kutoka asilimia 18 hadi 16 na sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia Septemba mosi mwaka huu.

“Kwa hiyo badala ya kutozwa asilimia 18 watatozwa 16 hivyo ni pungufu ya asilimia mbili hii ni kubwa sana katika mchakato wa kununua bidhaa,sheria inatutaka hadi tarehe hiyo iwe tayari kila kitu kimekamilika hivyo nawahaidi tutawatafuta wataalamu ilikuhakikisha jambo hili linafanikiwa,”amesema Mwenda.
Ameongeza,”Tunaandaa mifumo na tutasema ni akina nani wanafaidika na utekelezaji wake utakuwaje haya ni mapinduzi makubwa sana na yamelenga kupunguza matumizi ya fedha taslimu nchini niweke wazi kuwa punguzo hili linawahusu wale watakaolipa kidijiti ikiwemo simu lakini wale watakaotumia pesa taslimu wataendelea kulipa asilimia 18,”
Mwenda amesema walifanya mabadiliko ya sheria katika kifungu cha 51 na kuelekea maana ya biashara mtandaoni zinazokuongeza shughuli zote zinazofanywa kwa njia ya mtandao na walitoa ukomo wa kujisajili ambao ni Agosti30 mwaka huu.
“Nimesikia sauti zao kila sehemu na wengi wakihitaji zaidi kutoa elimu nikweli tunafikiria kuongeza muda lakini si kwa wamiliki na wanaopangisha nyumba kupitia Airbnb wala majukwaa ya kidigitali kama Kikuu, Netflix, Facebook, Instagram, Airbnb, Booking.com na Expedia hawa ni lazima ikifika tarehe mosi ni lazima watuchangie,”amesema Mwenda.

Amesema watafikiria kwa wa wengine kw ajili ya kuwasajili na kuwapa elimu kwani biashara za mitandao zimegawanyika lakini rasmi wataanza na wamiliki kwani wao wanapata pesa kutokana na watu kwenda maeneo mengine na hawachangii chochote hiyo si sawa .
Amesema ni kweli viwango vya kodi ni vikubwa na yeye anatamani vishuke lakini ili vishuke lazima uwe na njia mbandala ya kupata pato la kuisaidia serikali kama inawezekana kukusanya kidogo kidogo kwa wingi kikatosha kuendesha serikali hakuna sababu ya kuwa na tozo kubwa kiasi hicho na ni vyema jamii ikatambua kuwa wapo hapo kwa sababu kunawatu wanalipwa mishahara ya kuwalinda na inatokana na kodi.

Akizungumzia malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu mashini za EFD kuwa na gharama kubwa kushindwa Mwenda amesema kwa sasa Teknolojia imekua kila kitu kinapatikana kupitia simu za mkononi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo Severin Mushi amesema awali biashara za mitandao zili waadhiri wauzaji wa madukani kwani wao walikaa kusubiri wateja huku wenzao wakiwafua wateja hivyo kufanya biashara kuwa ngumu.
Aidha ameiomba TRA kukaa na TCRA kwa pamoja kujadili suala la kusitishwa kwa mtandao hili hali muda wa kodi unapofika inatakiwa kulipa haijalishi mauzo waliyonayo.








