KWA mujibu wa tathmini ya mashirika ya ujasusi ya Marekani, Iran imeongeza kwa kiasi kikubwa juhudi za kuwalenga wanadiplomasia na maafisa wengine wa Marekani katika Mashariki ya Kati na maeneo mengine duniani.

Inadaiwa kuwa mpango wa Iran umefikia kilele chake.

Kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani imetolewa wakati Washington ikipunguza idadi ya wanadiplomasia wake walioko katika moja ya nchi za Mashariki ya Kati.

Rais Donald Trump amesema Marekani inafikiria kuchukua hatua mpya za kijeshi dhidi ya Iran.

Kauli ya Trump inatolewa wakati Marekani na Israel zimekuwa katika vita na Iran kwa karibu miezi minane, huku kupanda kwa bei ya mafuta kukitarajiwa kuathiri uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani.

“Tunaweza kufanya operesheni nyingine ndogo kama Epic Fury, au wao (Iran) wanaweza kufikia makubaliano,” Trump alisema katika mkutano wa kampeni huko Florida, Ijumaa, Oktoba 23.

Aliongeza kuwa iwapo viongozi wa Iran wangekuwa na busara, wangesema: “Tuanze mazungumzo ya dhati.” Hata hivyo, Trump alisema ana shaka kama uongozi wa Iran una busara hiyo.

Operation Epic Fury ndilo jina linalotumiwa na jeshi la Marekani kurejelea vita dhidi ya Iran.

Katika hotuba yake, Trump alitetea tena uamuzi wake wa kuiondoa Marekani katika mkataba wa nyuklia wa Iran (JCPOA) wakati wa urais wake.

Alidai kuwa Marekani iliharibu uwezo wa Iran wa kurutubisha urani kupitia operesheni ya Midnight Hammer, na baadaye kuisababishia Iran uharibifu zaidi kupitia operesheni ya Epic Fury.

Trump alisema Marekani imeishambulia Iran kwa pigo kubwa, akidai kuwa uchumi wa nchi hiyo kwa sasa unakabiliwa na mojawapo ya hali ngumu zaidi duniani.

Mapema Ijumaa, Trump alisema pia kuwa vita dhidi ya Iran vinaweza kumalizika hivi karibuni. Hata hivyo, aliibua swali la iwapo Washington inapaswa kujaribu kumaliza vita mara moja au kuviacha vikome taratibu.

Trump amekuwa akitoa malengo na ratiba tofauti za kumaliza vita katika nyakati mbalimbali. Mapema Oktoba, alisema Marekani haitafanya shambulio jipya dhidi ya Iran kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Bunge, uliopangwa kufanyika Novemba 3.