Jana August 18, 2018 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amefariki jana Agosti 18 nchini Uswisi akiwa na umri wa mika 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Inaelezwa kuwa Annan ambae alikuwa ni Raia wa Ghana anatajwa kuwa Mtu wa kwanza mweusi kutoka Afrika kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoka mwaka 1997 mpaka mwaka 2006.

Annan ambae aliwahi kutunukiwa tuzo ya Nobel Peace atakumbukwa kwa mambo mengi ikiwemo kutatua mzozo uliotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwaka 2007.

Bado haijaelezwa ni lini na wapi Kiongozi huyo wa zamani wa UN atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Please follow and like us:
Pin Share