Mcheza filamu, raia wa Kenya, Lupita Nyong’o ameungana na wacheza filamu wengine Weusi kushutumu kutojumuishwa kwa wacheza filamu weusi au wale wachache kutoka kwa orodha ya wale wanaowania tuzo za Oscar.

Katika akaunti yake ya Istagram Lupita amesema amekasirishwa sana na kukosa kujumuishwa kwa wacheza filamu weusi. Hivyo, anasema hatahudhuria tuzo za Oscar.

Mwaka 2014 Lupita Nyong’o alishinda tuzo la Oscar kutokana na wajibu wake katika filamu ya Twelve Years a Slave.

Anaungana na wacheza filamu wanaozidi kuongezeka wakiwemo David Oyelowo na Don Cheadle ambao wamekosoa tuzo za Oscar kuwa kukosa kuteua watu kutoka tabaka zote.

Kuona hivyo, waandalizi wa Tuzo za Oscar wameahidi kuwa wataimarisha juhudi zao za kuongeza wanachama zaidi wanawake na watu wa kutoka katika jamii za wachache kama vile watu weusi ifikapo mwaka 2020.

Marekebisho yamefanywa baada ya juma moja la lawama baada ya kukosa washindi weusi walioorodheshwa kutangazwa katika hafla ya shughuli hizo mwezi ujao.

Waigizaji na waandalizi kadha wa filamu kama vile mwigizaji Will Smith na mwandalizi mkuu Spike Lee wamesema kuwa watasusia hafla za tuzo za Oscar mwaka huu kwa kuwa wote walioteuliwa ni wazungu.

By Jamhuri