Na Lookman Miraji,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Historia ya Uhuru wa taifa la India ilianzia katika kipindi cha ukoloni ambapo taifa hilo lilipata kutawaliwa na waingereza kuanzia miaka ya 1858 mpaka mwaka 1947 ambapo utawala wa muingereza ulitamatika rasmi kupitia mfumo rasmi wa mazungumzo ya Amani.

Kuanzia mwaka 1858 Uhindi ulitawaliwa kama koloni la Uingereza. Kaisari wa mwisho wa Moghul Bahadur Shah Zafar II aliondolewa nchini. Malkia Viktoria wa Uingereza alichukua cheo chake akaitwa “Kaisari wa Uhindi” (kwa Kiingereza: “Empress of India”; kwa Kihindi: “Padishah-e-Hind”) na kisha akamuachia utawala gavana wake aliyepewa cheo cha “makamu wa mfalme” aliyeitwa (Vice-Roy).

Muundo wa utawala uliendelea na maeneo ya kampuni yalikuwa makoloni ya Uingereza. Maeneo ya watawala Wahindi yalibaki kama yalivyo lakini kila Maharaja au Nawab alipaswa kula kiapo cha utii kwa malkia kama Kaisari au malkia mkuu wa Uhindi na kumkubali mshauri Mwingereza katika jumba lake kama mwakilishi wa Uingereza.

Mwishoni mwa karne ya 19 harakati za kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru. Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda “Shirikisho la Waislamu”.

Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu.

Mohandas Karamchand Gandhi maarufu zaidi kwa jina la Mahatma Gandhi, alikuwa mwanasheria, mwanafalsafa, mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa siasa nchini Uhindi.

Mahatma Gandhi anajulikana hasa kama kiongozi wa harakati za uhuru wa Uhindi aliyepinga na kushinda ukoloni kwa njia ya amani bila ya matumizi wa mabavu au silaha.

Gandhi alizaliwa mnamo Oktoba 2 ya mwaka 1869 huko nchini India.Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Na mnamo Agosti 15 mwaka 1947 taifa la India lilipata Uhuru wake tokea katika utawala wa waingereza. Mara baada ya hatua hiyo Swali kubwa lilikuwa, kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.

Ndani ya uhindi yenyewe fitina ilianzia juu ya nafasi ya waislamu katika taifa jipya , huku sehemu kubwa ya waislamu wakidai kugawiwa kwa koloni katika nchi mbili.

Katika hoja hiyo mapigano yalianza na watu elfu kadhaa waliuawa. Mnamo mwezi Agosti mwaka 1947 nchi mbili za Uhindi na Pakistan zilianzishwa ,na Oktoba 1947 vita vikafuata kati ya nchi hizo mbili juu ya jimbo la Kashmir. Vita hiyo vikaongeza uadui, na watu milioni kadhaa walifukuzwa yaani wahindu kutoka Pakistan na waislamu kutoka uhindi.

Mahatma Gandhi alijitahidi kupatanisha viongozi wa pande zote akitangaza alikuwa tayari kufungua hadi kifo kama endapo wasipopatana. Heshima kwa kiongozi huyo aliyekuwa akiheshimika sana na jamii ya Wahindi ilisababisha viongozi wa pande mbalimbali katika uhindi kukutana na kutafuta njia ya kumaliza uhasama huo uliokuwa ukiendelea kati yao.

Mnamo tarehe 30 januari mwaka 1948 kiongozi wa jamii ya wahindi Gandhi aliuawa kwa kupigwa risasi na kuuawa wakati akitembea katika bustani ya nyumba huko mjini Delhi nchini India.


Kwa mujibu wa tafiti zinasema kuwa muuaji aliyemuuwa kiongozi huyo alikuwa ni mhindu wa kundi lililofuata itikadi kali ambapo alikuwa akiamini hatua za kupatanisha waislamu na wahindu ulikuwa ni usaliti utakaofanywa na kiongozi Mahatma Gandhi.

Kwa mwaka huu 2024 taifa la India linaadhimisha miaka 78 ya uhuru wake. Sherehe hizo ambazo kitaifa zimeongozwa na Rais wa taifa hilo Droupadi Murmu huko nchini India.

Katika hotuba rasmi iliyotolewa na Rais Murmu ikiwa ni salamu za sikukuu hiyo ya taifa la India. Miongoni mwa mambo muhimu ambayo Rais Murmu amegusia katika hotuba hiyo rasmi ni kwa namna ambavyo uchumi wa taifa hilo unavyozidi kuimarika siku hadi siku.

”Kutoka mwaka 2021 mpaka mwaka 2024 India imekuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa Kasi ikiwa na wastani wa asilimia 8 kwa kila mwaka. Hili halijasaidia tu kutengeneza pesa zaidi isipokuwa imepunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watu waishio katika mazingira duni ya umasikini.” Amesema Rais Droupadi Murmu.

Aidha pia Rais Murmu amegusia juu ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali yake katika kuendelea kupambana na umaskini nchini humo.

”Na kwa wale ambao bado wanaishi katika mazingira duni jitihada kubwa zinaendelea kufanyika sio tu kuwapa msaada ila kuwatoa kabisa katika wimbi hilo umaskini.” Aliongeza Rais Murmu.

Shughuli hizo kwa hapa nchini zimeadhimishwa asubuhi ya leo Agosti 15 katika Ubalozi wa India ulioko DSM.

Maadhimisho hayo yaliongozwa na Balozi wa India nchini Bishwadip Dey ambapo aliungana na raia wengine wa India waishio nchini pamoja na waalikwa wengine.

Maadhimisho hayo yalienda sambamba pia na zoezi la ushushwaji wa bendera ya taifa hilo ikiwa na maana ya kuwa taifa hilo liko huru.

Please follow and like us:
Pin Share