Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema Kyiv haijawahi kuonyesha nia ya kurejea kwenye mazungumzo kati ya Urusi na wajumbe wa taifa hilo.

Peskov alisema hayo katika mahojiano na Shirika la habari la serikali la Urusi RIA yaliyochapishwa siku ya Jumatatu.

Peskov alisema hayo alipoulizwa ikiwa kuna uwezekano wa kurejea kwenye mazungumzo na wajumbe wa Ukraine na kuongeza kuwa hadi sasa hakuna dalili yoyote ya msingi kutoka kwa Kyiv.

Mjini Moscow aidha, taarifa zimesema mji wa Belgorod umejikuta gizani baada ya umeme kukatika kufuatia shambulizi lililofanywa na Ukraine hiki kikiwa kisa cha kwanza kikubwa tangu kuanza kwa vita kati ya Urusi na Ukraine.