Mgombea ubunge Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Sh bilioni 97 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la juuu katika eneo la Jangwani, Dar es Salaaam.
Ulega ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kusalimia maelfu ya wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Leaders Club leo Oktoba 21,2025.
Amesema ujenzi utasaidia kiasi kikubwa kuondoa msongamano wa foleni na kuepuka tatizo kubwa la mafuriko.
Amesema Rais Samia ametoa Sh trilioni 1.7 katika Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Watanzania wanakupenda ndiyo maana Dar es Salaam umenufaika na uongozi wako. Huu mji siyo ule miaka 10 iliyopita.
“Nimesoma hapa tulikuwa tunagombania usafiri kutoka Mbagala kuja shuleni, lakini sasa hivi hakuna shida hiyo tena,
“Umetoa maelekezo ya kuondoa msongomano ulitupatia maagizo makubwa mawili.
“Mosi kuondoa msongamano kwa sababu muda mwingi unapotelea kwenye foleni
“Pili fedha ya kuondoa mafuriko ipo, ndiyo maana tunasema una utu unagusa maisha ya Watanzania.
“Kila daraja au kilomita moja inayojengwa inakwenda kunusuru utu wa Mtanzania ndiyo maana wanakupenda sana Oktoba 29, wanakwenda kukuchagua,*amesema.
