WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Agnes Meena kumsimamisha kazi Afisa Mfawidhi anayeshughulikia ubora wa samaki kituo cha Kigoma, Bw. Frank Kabitina kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Ulega ametoa maelekezo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi katika Mwalo wa Katonga Mkoani Kigoma Januari 9, 2024.

Alisema afisa huyo amekuwa akikusanya mapato ya mazao ya uvuvi na sehemu ya mapato hayo akiyatumia kwa manufaa yake binafsi.