Home Michezo UNAJUA KWANINI LIVERPOOL WALIMUUZA COUTINHO, SOMA HAPA

UNAJUA KWANINI LIVERPOOL WALIMUUZA COUTINHO, SOMA HAPA

by Jamhuri

Meneja wa Timu ya Liverpool, Jurgen Kloop ameeleza kuwa klabu yke ilifanya kila iwezalo ili kuendelea kuwa na mchezaji Phillipe Coutinho, lakini mwisho wa siku mchezaji huo raia wa Brazili alikuwa na tamaa ya kwenda kuichezea Klabu ya Barcelona.
Hatimaye kiungo huyo mkabaji, Phillipe Coutinho amekamilisha kusaini mkataba uliokuwa ukisubiriwa sana na klabu ya Barcelona.
Juzi Jumamosi, Januari 6, 2018 Coutinho aliondoka katika dimba la Anfield kuelekea Camp Nou kwa dili la pauni milioni 142, sawa na shilingi za kitanzania bilioni 431.3, kiwango ambacho kinamfanya mchezaji huyo kushika nafasi ya tatu katika orodha ya wachezaji gali zaidi duniani.
Klabu ya Liverpool, kupitia Meneja wake, Kloop imeeleza kuwa ilifanya kilka namna ili kubaki na mchezaji huyo lakini hawakuwa na la kufanya na mwisho wa siku ilibidi wamruhusu aondoke.

You may also like