KUTOKANA na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa ahadi za ufadhili, Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) limepunguza takriban wafanyakazi 5,000 duniani kote mwaka huu

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwashughulikia Wakimbizi, Filippo Grandi alisema mjini Geneva kwamba hatua hiyo inamaanisha kuwa robo ya wafanyakazi wote wamepoteza ajira zao.

Hadi Juni 2024, UNHCR ilikuwa na takriban wafanyakazi wa kudumu 15,400 na wadau wengine 4,400 katika zaidi ya nchi 130, na kufanya jumla kufikia karibu 20,000. Mwishoni mwa mwaka, shirika hilo la misaada linatarajiwa kuwa na takriban dola bilioni 3.9, kiasi ambacho ni robo pungufu ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kutokana na hali hiyo, shughuli mbalimbali za UNHCR tayari zimesitishwa, ikiwemo programu za kusaidia waathirika wa mateso. Shule zimefungwa na msaada wa chakula na fedha kwa wakimbizi umepunguzwa.