Matokeo ya uchaguzi Mkuu kenya huenda yakatolewa leo kama zoezi la kuhesabu kura litakamilika kutoka kwa kaunti zote.

Kati ya wagombea wanne wa kiti cha urais nchini humo ni wagombea wawili wanaonyesha ushindani mkali kwa kukabana kwa idadi ya kura nyingi katika baadhi ya kaunti tofauti tofauti kulingana na ushawishi walonao katika kaunti hizo.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yanayoendelea kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini humo mgombea urais kwa tiketi ya Muungano wa Kenya kwanza William Somei Ruto anaongoza kwa asilimia 50.9 huku mshindani wake kwa ticket ya Azimio La Umoja Raila odinga akiwa na kura asilimia 48.5

Hadi kufikia sasa wagombea walio wengi katika nafasi za ugavana, Seneta na ubunge wamekwisha kusherekea ushindi wao kutokana Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya IEBC kuwatangaza kama washindi katika nyadhifa hizo huku wanasiasa wanawake wakichomoza pia.

Tumme huru ya Uchaguzi na Mipaka inatarajia kuwatangazia Wakenya Rais wao kabla ya siku saba kutimia kama ulivyo utaratibu wa kikatiba nchini humo, na ili Mgombea kushinda duru ya kwanza ya uchaguzi huo lazima apate kura asilimia 50 na moja zaidi na takribani asilimia 25 ya kura za kaunti 24 kati ya kaunti 47

Kati ya wakenya milioni 22 waliojiandiisha kupiga kura nchini Kenya ni takribani wakenya Milioni 13 waliojitokeza kupiga kura jumla ya wapiga kura milioni 8.8 wakiwa ni vijana sawa na asilimia 39.84 idadi hiyo ya wapiga kura vijana ikishuka kwa asilimia 5.17 ukilinganisha na ile ya mwaka 2017

Aidha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya imefanya zoezi la wazi patika mchakato wa kupiga na kuhesabu kura na vyombo nya habari vimekuwa huru kuripoti kulingana na hali inavyoendelea.

Fuatilia zaidi matokeo ya uchaguzi mkuu Kenya kwa kugusa hapa

By Jamhuri