Waokoaji wameanza harakati za uokoaji wa manusura baada ya bwawa kupasuka siku ya Jumatatu jioni , na kusababisha mafuriko yaliowauawa watu 20 katika vijiji

Takriban watu 100 wametoweka na maelfu kupoteza makao yao.

Mamlaka katika mkoa wa Attapeu imekuwa ikitumia ndege aina ya helikopta na maboti ili kujaribu kuwaokoa wanakijiji waliokwama.

Bwawa hilo lililopasuka ni miongoni mwa mradi wa umeme wa Xe-Pian Xe-Namnoy unaohusisha Laotian, Thai na kampuni za Korea kusini.

Mamlaka imeomba serikali na jamii nyengine kutoa usaidizi wa dharura kama vile nguo za kuvaa, chakula, maji ya kunywa na dawa.

Kanda za video za mkasa huo zimeonyesha vile manusura walivyolazimika kupanda katika paa za nyumba zao zilizomezwa na maji hayo , ama kutembea katika maji wakiwabeba watoto na mali zao.

Mwanamke mmoja, aliyeonekana katika kanda ya video iliochapishwa na chombo cha habari cha Laos ABC katika mtandao wa Facebook akilia na kuomba alipokuwa akiokolewa akiwaambia waokoaji kwamba mamake bado amekwama juu ya mti.

Bwawa lililovunja hilo lililovunja kingo zake hutumika kusafisha maji yanayoingia katika bwawa kuu na linaitwa “Saddle Dam D”.

Ni miongoni mwa mabwawa matano katika mradi huo wa umeme wa Xe-Pian Xe-Namnoy .

Bwawa hilo lilikuwa limekamilika asilimia 90 na lilikuwa linatarajiwa kuanza operesheni za kibishara mwaka ujao.

Kampuni ya SK Engineering & Construction, inayomilikiwa na Korea Kusini ilisema kuwa mwanya ulionekana katika bwawa hilo siku ya Jumapili kabla ya kuvunja kingo zake.

Kampuni ya umeme ya Ratchaburi Electricity Generating Holding, ambayo ndio mshikadau mkuu wa mradi huo , ilisema katika taarifa kwamba bwawa hilo lilipasuka kutokana na mvua kubwa iliosababisha maji mengi kuelekea katika bwawa hilo.

Laos katika miaka ya hivi karibuni iliwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika mradi huo wa umeme-ambao unachangia asilimia 30 ya biashara yake ya nje

Serikali inapanga kuongeza maradufu uzalishaji wake wa umeme kufikia 2020 ili kuwa tegemo la umeme kusini mashariki mwa Asia”.

Lakini makundi yameonya kuhusu athari ya mradi huo kwa mazingira

Please follow and like us:
Pin Share