Wanasayansi wameonya leo kwamba karibu watu bilioni 3.8 duniani, huenda wakakabiliwa na joto kali zaidi ifikapo mwaka 2050 huku nchi za ukanda wa Tropiki zikitarajiwa kuathirika zaidi.

Wanasayasni wameonya leo kwamba karibu watu bilioni 3.8 duniani, huenda wakakabiliwa na joto kali zaidi ifikapo mwaka 2050 huku nchi za ukanda wa Tropiki zikitarajiwa kuathirika zaidi.

Kwa mujibu wa wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, ongezeko la wastani la siku zenye joto kali linaweza kuwa na athari kubwa katika nchi ambazo hazijazoea hali hiyo kama vile Canada, Urusi na Finland.

Mahitaji ya vifaa vya kupozea hewa yataongezeka kwa kiwango kikubwa katika nchi kama Brazil, Indonesia na Nigeria, ambako mamilioni ya watu hawana viyoyozi au njia nyingine za kujikinga dhidi ya joto.

Utafiti huo mpya, ulizingatia hali tofauti za ongezeko la joto duniani ili kutabiri ni mara ngapi, katika siku zijazo, watu wanaweza kukumbana na viwango vya joto vinavyochukuliwa kuwa vya kupindukia iwe ni joto au baridi kupita kiasi.