Watua nchini Uingereza kupinga uhifadhi Loliondo

Ujumbe wa watu watano kutoka Loliondo, Tanzania na nchini Kenya, upo nchini Uingereza kuchangisha fedha za kuendesha harakati za kupinga mpango wa serikali wa kutenga eneo la hifadhi ndani ya Pori Tengefu la Lolindo.

Hivi karibuni Gazeti la JAMHURI liliandika kuhusu safari ya Watanzania kadhaa nchini Uingereza wakilenga kupata fedha za kuendeshea harakati za kupinga mpango huo wa uhifadhi.

Watu hao watatu walipita Namanga kabla ya kwenda kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Wametambuliwa kuwa ni Samwel Naingirya, Diwani wa Ololosokwan; Yanik Ndoinyo na Shomet Naigisa. Wamekwenda kama wawakilishi wa asasi (NGO) ya TEST iliyosajiliwa nchini Kenya.

TEST inafanya kazi zake Kaskazini mwa Tanzania na sehemu chache za Kenya katika County ya Narok, lengo likiwa kujenga mshikamano kwa ajili ya kulinda ‘ardhi ya Wamasai’ bila kujali mipaka ya kimataifa.

Lengo la mkutano huo ni kutafuta fedha kutoka kwa NGOs na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na utetezi wa ardhi ya wenyeji.

Nangirya anawakilisha Oltoilo le Maa, ambao shughuli zao ziko katika Msitu wa Enguserosambu, Kata ya Orgosorok ambako wanaendesha miradi ya uhifadhi na utalii.

Mpango mkakati wa safari hiyo ni maandalizi ya kupinga mpango wa serikali wa kutenga eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 1,500 kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji, ushoroba (mapito ya wanyama) na eneo la mazalia ya nyumbu na wanyamapori wengine. Ziara hiyo itawawezesha, pamoja na wadau wengine, kukutana na kufanya mazungumzo na asasi ya Avaaz ambayo imekuwa mstari wa mbele kupinga mipango mingi ya Serikali ya Tanzania kwa eneo la Loliondo.

Ukiacha suala la uhifadhi, asasi hiyo imesimama kidete kupinga ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu (Arusha) – Makutano (Mara) inayolenga kupunguza adha kwa Watanzania