Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Mannyara
WAZIRI wa Viwanda na Biashara hapa nchini Seleman Jafo amempongeza Wakili Msomi na Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara kwa kufanya kazi kubwa sana ya kulielimisha Bunge la Tanzania kupitia ELIMU yake ya USOMI wa SHERIA
Jafo ameyasema hayo Jana Bungeni wakati akipokua akizungumza juu ya uwekezaji mkubwa a kiwanda Cha simenti kitakachotarajiwa kuwekezwa Kanda ya katika, ambapo mbunge Lekaita alitaka kujua kama ni lini Waziri Jafo atawapeleka wawekezaji hao Kiteto kwakua wapi tayari kuwapokea.
Jafo amesema ELIMU yake ya usomi wa Sheria imewaaidia sana kama Bunge la Tanzania, ambapo amewataka watu wa Manyara kutambua hilo kuwa Wana Mbunge makini kutoka katika wilaya ya Kiteto.
Aidha Jafo amesema anamuombea ili wananchi wa Kiteto waweze kumrudisha Bungeni kwani amekua ni msaada mkubwa sana
” Naomba nikupongeze kwanza Wakili Msomi kaka yangu Edward Ole Lekaita, nakuombea sana watu wa Kiteto wakurudishe, Umefanya kazi kubwa sana, Umelielimisha Bunge hili sana , Elimu yako ya Usomi wa Sheria imetusaidia sana kama Bunge la Tanzania, na watu wa Manyara wasikie kwamba tuna Mbunge makini kutoka katika wilaya ya Kiteto ” amesema Waziri Jafo.
Aidha Waziri Jafo akijibu swali kutoka Kwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Wakili Msomi Edward Ole Lekaita la ni lini atawapeleka wawekezaji hao Kiteto, Jafo amesema wawezaji watapita katika maeneo ya Kanda ya kati hayo watafanya kuangalia ni wapi patastahili kujengwa kiwanda kikubwa cha simenti, ambapo watahakikisha maeneo yote wanayapitia.
” Lakini naamini katika Kanda hii ya katikati tukipata kiwanda kiwanda kimoja kikubwa Provided sehemu yoyote kitakapojengwa kutasaidia Wananchi wa Kanda hii” amesema Jafo.
” Kwahiyo ni imani yetu kama Serikali tutahamasisha kupata watu hawa wafike maeneo haya waweze kuwekeza, kwahiyo naomba niwahakikishie watu wa Manyara na Dodoma kuwa tunaangaika ujenzi wa kiwanda kikubwa cha simenti hapa kwa lengo kubwa kwamba itumie hii mikoa kuzalisha malighafi ya simenti” amesisitiza Waziri Jafo.
