Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amewataka Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa na Wilaya (RTOs na DTOs) kuendelea kuwachukulia hatua kali madereva sambamba na watumiaji wengine wa vyombo vya moto wasiotaka kufuata sheria,kanuni na alama za usalama barabarani ambao wamekuwa chanzo cha kusababisha ajali zinazoendelea kujitokeza.

Sagini amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha kufanya tathmini ya utendaji kazi, mafanikio na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wanapotekeleza jukumu la kusimamia sheria za usalama barabarani, kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma na kuwahusisha Wakuu wa usalama barabarani wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makao Makuu ya Kikosi.

Kikao kazi hicho cha siku tatu kinatarajia kutoka na mikakati ya kupunguza ajali za barabarani, kuondoa malalamiko kutoka kwa watumiaji wa barabara kwa kuwatendea haki kwa mujibu wa sheria na kuwa na mpango kazi wenye tija katika kusimamia askari na sheria za usalama barabarani.

By Jamhuri