Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,Amir Abdollahian aliwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam

Mara baada ya kuwasili nchini, Abdollahian amesema, lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Iran na Tanzania katika sekta za kisiasa na kiuchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.  Mhe. Abdollahian aliwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. 

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alimueleza nia ya Serikali ya Tanzania ni kuendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imejidhatiti katika kukuza na kuendeleza Diplomasia ya Uchumi hivyo ni matumaini yake kuwa ujio wake hapa nchini utachangia kuendeleza diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Iran.

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian yakiendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza.

By Jamhuri