Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limetahadharisha kwamba maradhi ya homa ya nyani bado ni kitisho cha kiafya kote ulimwenguni bila kujali mipaka.

huku likielezea wasiwasi wake kwa kuangazia hasa mlipuko wa aina mpya na mbaya zaidi ya virusi vya homa hiyo, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

WHO limesema mwezi uliopita pekee, lilipokea ripoti za visa kutoka nchi 26 na Mkurugenzi wake, Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari kwamba kitisho bado ni dhahiri.

Amesema, mlipuko huo hauonyeshi dalili ya kupungua, wakati kukiripotiwa visa 11,000 mwaka huu, pamoja na vifo 445, huku watoto wakiathirika zaidi.

Rosamund Lewis, anayeongoza jopo la ufundi la WHO linaloshughulikia maradhi hayo, naye amesema wana wasiwasi sana na hali hiyo