Zaidi ya wagonjwa 160 wanapokea matibabu katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kufuatia maandamano ya jana ya kupinga ushuru.

Kaimu mkuu wa upasuaji katika hospitali hiyo Dk Benjamin Wabwire anasema wagonjwa wengi waliletwa wakiwa na majeraha mbalimbali , sita walikuwa na majeraha ya risasi na 20 waliojeruhiwa kutokana na risasi za mpira.

“Kwa aina ya majeraha tunayotibu, hii ni idadi kubwa sana.” Wagonjwa 72 wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku 23 wakisubiri upasuaji wa baadaye ‘

Hospitali hiyo pia ilipokea wagonjwa 15 kutoka mtaa Githurai,viungani mwa jiji jana usiku, ambapo kulikuwa na madai ya ukatili wa polisi.

Watu wanane kwa sasa wanafanyiwa upasuaji mbalimbali.

Hospitali imerekodi vifo vitatu: miili miwili iliyoletwa hospitalini na mtu mmoja aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu