…………………………………………….

Klabuya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu kwa kuweza kuinyuka KMC FC 5-0, kwenye mchezo wa ligi Kuu NBC uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam.

Katika Mchezo huo Yanga iliwaanzisha baadhi ya nyota wao akiwemo Pacome Zouzoua ambaye amekuwa nyota wa mchezo kwa kufanikiwa kufunga bao moja na kutengeneza lingine kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi mnono.

Zouzoua ameonesha uwezo wake na kuvuta hisia za mashabiki ambao walifika uwanjani wakishangilia pindi anapogusa mpira  na kupeleka mashambulizi kwa wapinzani.

Dickson Job alianza kuandika bao la kwanza kipindi cha kwanza mara baada ya kupiga shuti la kisigino kipa wa KMC na kuokoa hivyo Job akapata nafasi tena ya kufunga bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Mabao mengine ya Yanga Sc yamewekwa kimyani na Mudathir Yahya, Aziz Ki pamoja na KonKoni.