Monthly Archives: June 2019

Mwendokasi usitufunze chuki

Kama hamfahamu, Mpita Njia, maarufu kama MN ni mtumiaji mzuri wa usafiri uendao haraka (mwendokasi) mara kwa mara anapokuwa katika Jiji la Dar es Salaam. Kwa takriban miaka miwili ambayo amekuwa mtumiaji mzuri wa huduma ya usafiri huo amezishuhudia tabia nyingi za watumiaji wa usafiri husika. Kama ukifanyika utafiti wa mabadiliko ya kitabia kwa watu wanaotumia usafiri huo, hakika kwa ...

Read More »

Chanzo kipya kodi tril. 23/- hiki hapa

Wakati mjadala wa bajeti ya Sh trilioni 33 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ukiendelea bungeni, JAMHURI limeelezwa kuwapo kwa chanzo kikubwa kipya cha mapato kilichopuuzwa kwa miaka takriban mitatu. Wataalamu wa masuala ya soko la mtandaoni wanasema Tanzania ikiwekeza katika uendelezaji wa soko la mtandao, inaweza kupata hadi dola bilioni 10 kama kodi, sawa na Sh trilioni 23. “Ni bahati ...

Read More »

Ubakaji watoto wakubuhu Same

Matukio ya kubakwa watoto wa kike wenye umri chini ya miaka 18 katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro yanaongezeka licha ya baadhi ya washitakiwa kufungwa jela. Taarifa zinaonyesha kuwa kati ya Januari, mwaka jana hadi Mei mwaka huu, mashauri 34 yamefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same. Washitakiwa watatu kati ya hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja; ...

Read More »

Upanuzi Bandari ya Dar kuongeza ufanisi

Serikali inaendelea kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia shehena kubwa zaidi. Katika maboresho hayo magati 1-7 yanafanyiwa ukarabati pamoja na ujenzi wa gati jipya litakalohudumia meli zenye shehena ya magari. Maboresho hayo ambayo yako chini ya mradi wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project (DMGP), yana umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na nchi ...

Read More »

Tunahitaji utulivu mjadala wa bajeti

Alhamisi wiki iliyopita serikali kupitia kwa Waziri wa Fedha iliwasilisha mapendekezo ya bajeti kuu kwa ajili ya mwaka wa fedha 2019/2020. Bajeti hiyo baada ya kuwasilishwa itajadiliwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao kwa mujibu wa taratibu watakuwa na fursa ya kufanya marekebisho kwa kadiri watakavyoona inafaa kwa kuzingatia masilahi ya taifa. Katika mapendekezo ya ...

Read More »

NINA NDOTO (22)

Kupuuza ubunifu ni kuua ndoto   Kila mmoja wetu amezaliwa na ubunifu ndani yake, jambo hili lipo wazi hasa pale tunapowatazama watoto wadogo. Tukiwa watoto tunaweza kufanya mambo mengi na kujaribu vitu vingi. Watoto hutengeneza vitu kwa kutumia vifaa vinavyozunguka mazingira yao. Atajenga nyumba kwa kutumia miti, au anatumia kijiti kujifunza kuchora. Au anatumia makopo kama vifaa vya jikoni, atatengeneza ...

Read More »

Dawasa inavyoimarisha miundombinu ya maji

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imewakosha viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam kwa namna inavyotekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015. Dawasa inatekeleza miradi mikubwa ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kwa kutumia fedha zake. Hiyo ni hatua kubwa katika kuwafikishia maji wananchi kupitia kaulimbiu ya ‘Kumtua mama ...

Read More »

PSSSF yatumia tril. 1.1/- pensheni

Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ndani ya miezi sita umetumia Sh trilioni 1.1 kulipa pensheni za wastaafu. Kiwango hicho kinajumuisha jumla ya Sh. bilioni 880 ambazo wamelipwa wastaafu 10,000 ambao pensheni zao zilisimamishwa katika Mfuko wa PSPF kupisha shughuli ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ya GEPF, LEPF na PPF, huku Sh bilioni 300 zikitajwa kulipwa ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (18)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kusema wiki hii nitaangalia taratibu na viwango vya kodi wanazolipa wafanyakazi walioajiriwa katika kampuni, taasisi au shirika, kisha ikiwa nafasi itaruhusu nitajadili kodi ya mashirika. Sitanii, kabla ya kuangalia kodi hizi naomba uniruhusu mpendwa msomaji nitumie fursa hii kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa bajeti iliyowasilishwa bungeni ...

Read More »

Butiku: Ni miaka 23 ya Nyerere Foundation

“Jengo hili litakuwa na ofisi za kudumu za Taasisi ya Mwalimu Nyerere, maktaba ya taasisi itakayotoa fursa kwa Watanzania na watu wengine wote kusoma maandiko na nyaraka mbalimbali alizoandika Mwalimu Nyerere, pamoja na shughuli za uwekezaji za wabia, hususan hoteli ya ngazi ya kimataifa.” Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) Juni 26, mwaka huu inatimiza miaka 23 tangu kuanzishwa kwake. Taasisi ...

Read More »

Ndugu Rais kwa hili mwanao ninakuunga mkono

Ndugu Rais umewaita wafanyabiashara Ikulu tambua makundi mengine nayo yanasubiri uwaite. Uamuzi wako wa kutumbua papo kwa papo uliwajengea baadhi matumaini. Ninakuunga mkono. Lakini uliowabadilishia wana tofauti gani na uliowaondolea? Mojawapo lililomuondoa Mwigulu Nchemba si Lugumi Enterprises? Mbadala wake kafanya nini? Bungeni hakusema Rais mwongo. Lakini kama baba kasema nguo hazipo, yeye anasema hajawahi kuona mwongo kama wanaosema sare hazipo, ...

Read More »

Bandari hailali, chukua mzigo wako saa 24/7

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kushirikiana na wadau wake wa bandari imeendelea kuboresha na kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wake katika Bandari ya Dar es Salaam. Uboreshaji huo unaendelea kufanyika kwa sababu bandari ni lango kuu la biashara kwa nchi yetu na nchi zote zinazotumia bandari hii kubwa hapa nchini. Kati ya mambo yaliyoboreshwa na yaliyorahisishwa katika ...

Read More »

Serikali hazina uwezo kumaliza matatizo yote

Narudia mada ambayo hunikosesha usingizi mara kadhaa kila mwaka: elimu. Mahsusi ni ugumu wa kuhimiza jamii kuchangia uboreshaji elimu. Ni suala ambalo nalikabili kila niwapo kazini kwa sababu ya nafasi yangu kama msimamizi wa asasi isiyo ya kiserikali inayogharimia mahitaji ya elimu ya watoto yatima na watoto 150 wanaoishi kwenye mazingira magumu Mkoa wa Mara ya Global Resource Alliance (GRA) ...

Read More »

Kumshitaki daktari aliyesababisha madhara au kifo

Wako watu wengi wameathirika kutokana na matendo yanayotokana na uzembe, kutojali au makusudi ya madaktari. Wapo waliopata vilema vya muda kutokana na uzembe huo, wapo waliopata vilema vya maisha na wapo waliouawa na madaktari. Ajabu ni kuwa ukifanya tathmini ya haraka utaona kuwa watu wote waliopata madhila kutoka kwa madaktari huhusisha madaktari wa serikali, katika hospitali za serikali.  Si rahisi ...

Read More »

Usiamini uwepo wa uchawi (3)

George Benerd Shaw alipata kuandika haya: “Maendeleo hayawezekani bila mabadiliko ya fikra na wale ambao hawawezi kubadilika namna wanavyofikiri hawawezi kubadili chochote.” Kila kukicha mwanadamu anakabiliwa na zoezi la kufanya uchaguzi fulani. Ulimwengu huu hauna nafasi kwa watu wanaopuuzia maarifa ya mhimu. Kila kukicha yeyote anaalikwa kuukaribisha utajiri na kuuaga umaskini au kuuaga utajiri na kuukaribisha umaskini. Methali ya Kichina ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (33)

Makosa ya wengine ni walimu wazuri Makosa ni mtihani. “Inabidi mtu awe mkubwa kiasi cha kukubali makosa yake, makini kiasi cha kuyafaidi na jasiri kiasi cha kuyasahihisha,” alisema R.B. Zuck. Tunajifunza mambo matatu. Kwanza, yule ambaye hakubali makosa yake bado ni mdogo. “Hakuna mtu ambaye amekuwa mkubwa bila kupitia makosa mengi na makubwa,” alisema Phyllis Bottome. Pili, ni kujifunza kutokana na ...

Read More »

Demokrasia na haki za binadamu – (2)

Juma lililopita niligusia kuasisiwa kwa demokrasia na kutangazwa rasmi tangazo la haki za binadamu. Leo naangalia baadhi ya changamoto zinazotokana na misamiati hii ya siasa, utawala na haki kwa wananchi wa Afrika. Nathubutu kusema tawala karibu zote duniani zinakiri kuheshimu na kufuata misingi ya demokrasia na kanuni za haki za binadamu. Lakini kuna dosari za makusudi za hapa na pale ...

Read More »

Yah: Mheshimiwa Rais watafute kina Magufuli

Natuma salamu nyingi sana kwako lakini najua inawezekana umekaa katika kiti na umeshika tama ukitafakari mambo yanavyokwenda, unaona mahali ambapo mambo yamekwama na kuna mteule wako yupo yupo, kama nakuona unampa muda wa kujitafakari ajue unataka nini lakini anashindwa, unamtumia meseji juu ya mambo yanavyokwenda lakini amekaa kimya au kuitisha kikao cha kujadili jambo ambalo wewe umeliona na ungedhani anapaswa ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (2)

Wiki iliyopita makala hii iliishia katika aya iliyosema: “Yule kizee aliyeniweka mlangoni alikuja akataka kunichukua tena anipeleke kusikojulikana. Nilikataa na akawa ananilazimisha nikubaliane naye. Hapana jamani, dunia ya Gamboshi ndiyo hasa ninayopenda kuishi, maisha ya maajabu ndiyo kipenzi cha roho yangu. Si unajua tena wahenga walisema kipenda roho kula nyama mbichi. Sasa huyu bibi ananipeleka wapi tena? Mimi ni Gamboshi ...

Read More »

Mitanange ya kibabe AFCON

Takriban siku tatu zimebaki kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kuanza rasmi mwaka huu. Katika michuano hiyo mechi nyingi zitachezwa katika makundi manne, na kila kundi hujumuisha timu nne. Kuanzia kundi A, ambalo linaongozwa na timu mwenyeji, timu ya taifa ya Misri hadi kundi F. Waandaaji wa mashindano hayo, Misri wakiwa katika kundi hilo la A, wataongozwa ...

Read More »

Polisi wamkoga JPM

Ni ajabu na kweli, magari matano kati ya manane yaliyokuwa yanahusishwa na ‘papa wa unga’, yaliyokuwa yamehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay yameondolewa kituoni hapo kwa njia za utata. Magari hayo ya kifahari ni mali ya Lwitiko Samson Adam (Maarufu kama Tikotiko), ambaye alikamatwa mwishoni mwa mwaka 2017 kisha kuachiwa kabla ya kukamatwa tena. Magari hayo ya kifahari ambayo yamekuwa kwenye ...

Read More »

Mdhamini, Mwenyekiti CWT

Hali imezidi kuwa tete katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT), baada ya baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho kutiliwa shaka na baadhi ya wanachama, JAMHURI limebaini.  Gazeti hili la JAMHURI limejiridhisha kuhusu kuwapo kwa mpasuko miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Katibu wa Bodi hiyo akipingana na wenzake kwa tuhuma kuwa wamekuwa wakilinda ‘uchafu’ unaokizonga ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons