Monthly Archives: August 2019

Bundi atua wizarani

Baada ya gazeti hili la uchunguzi, JAMHURI, kuandika kuhusu ubovu wa matrekta wanayouziwa wakulima nchini wiki iliyopita, Bunge kupitia Kamati ya Viwanda na Biashara limeingilia kati kunusuru nchi kuingia katika madeni yasiyo na faida, hivyo kumwita Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, ajieleze. Habari za uhakika kutoka bungeni zinaeleza kuwa Jumatano iliyopita uongozi wa Shirika la Maendeleo la Taifa ...

Read More »

Hii Barack Obama vipi?

Mpita Njia (MN) anawapongeza viongozi wote walioandaa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo umeshuhudia Rais John Magufuli akikabidhiwa kijiti cha kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo muhimu sana kwa nchi za kusini mwa Afrika. MN ameshuhudia kujipanga na kuendesha shughuli ya kuwapokea marais zaidi ya 10 kwa mpigo kwa ajili ya shughuli hiyo. Pamoja ...

Read More »

Bili za miili sokomoko Muhimbili

Baadhi ya ndugu hulazimika kutelekeza miili ya wapendwa wao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana hali ngumu ya uchumi, JAMHURI limeelezwa. Ndugu hao huchukukua hatua hiyo baada ya kushindwa kulipia gharama  za matibabu za mpendwa wao alipokuwa akiendelea na matibabu. Ofisa Ustawi wa hospitali hiyo, Emmanuel Mwasota, amesema idara yake imekuwa ikibeba mzigo huo kwa ajili kusaidia wanandugu wasio na uwezo wa kulipia ...

Read More »

Maji sasa ni anasa Mwanza

Maji ni anasa katika Jiji la Mwanza, hivyo ndivyo mtu anavyoweza kuelezea kulingana na ongezeko la bei ya maji katika Jiji la Mwanza. Ongezeko la bei ya maji kwa ndoo moja ya lita 20 imepanda kutoka Sh 14 hadi kufikia Sh 24.50. Yaani imeongezeka Sh 10.50 kwa kila ndoo. Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa, hili ni ongezeko la zaidi ya asilimia 70 kwa mwananchi. Baadhi ya ...

Read More »

Kushangilia wanaotuumiza ni kukosa uzalendo kwa nchi

Hadi tunakwenda mitamboni, ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ilikuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kutokana na amri ya mahakama. Sababu za kukamatwa kwa ndege hiyo bado hazijawekwa bayana, japo kuna maelezo kuwa hatua hiyo imetokana na serikali yetu kudaiwa. Hii si habari nzuri hasa kwa kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano imenuia kwa vitendo kuifufua ATCL, hivyo ...

Read More »

NINA‌ ‌NDOTO‌ ‌(32)‌

Jifunze‌ ‌kuamka‌ ‌mapema‌ “Kama una ndoto ya kuajiriwa, usilale hadi saa moja.”  alisema Ruge Mutahaba akiwa mkoani Mbeya katika fursa mwaka 2017. Linaweza kusikika kama jambo geni, lakini watu waliofanikiwa kwenye sekta mbalimbali ni watu waliojijengea tabia ya kuamka mapema. Msemo wa Ruge Mutahaba nilioanza nao hapo juu si tu maalumu kwa watu wanaotaka kuajiriwa ,  bali kila mtu anayetaka ...

Read More »

NMB yazidi kumwaga mamilioni sekta ya elimu

Benki ya NMB imekwisha kutoa kiasi cha zaidi ya Sh milioni 570 hadi sasa kati ya Sh bilioni 1 ilizotenga kama uwajibikaji wake kwa jamii kwa mwaka huu wa 2019. Kiasi hicho kimetumika zaidi kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii kama elimu, afya na kusaidia majanga mbalimbali yanayoipata nchi, ikiwa ni utaratibu wa benki wa kila mwaka kutenga asilimia moja ya ...

Read More »

HOTUBA YA MHESHIMIWA DK. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUFUNGA MKUTANO WA 39 WA WAKUU WA NCHI WA SADC DAR ES SALAAM, TAREHE 18 AGOSTI, 2019

Naomba nianze kwa kutoa taarifa. Jana, baada ya kusoma sehemu ya hotuba yangu ya ukaribisho kwa kugha ya Kiswahili; Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC walifurahi na kuvutiwa sana. Hivyo basi, tulipokwenda tu kwenye mkutano wetu wa ndani, wote kwa pamoja na kwa kauli moja, walifanya uamuzi wa kukifanya Kiswahili kuwa Lugha Rasmi ya Nne ya SADC. Hii ndiyo ...

Read More »

Maendeleo Bukombe yanavyokimbia (1)

Bukombe ni moja ya wilaya zinazopatikana katika Mkoa wa Geita. Wilaya hii inakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 8,055.59 huku asilimia 21.9 likiwa ni eneo la makazi (km. 1,766.59), eneo linalobaki ambalo ni kilometa za mraba 6,289 ni pori la hifadhi ya misitu na Hifadhi ya Kigosi Muyowosi. Wilaya hii pia inalo jimbo moja la uchaguzi ambalo ni ...

Read More »

Bandari Mtwara mlango muhimu SADC

SERIKALI ya Tanzania imekuwa ikiboresha bandari nchini kote ikilenga kurahisisha huduma za usafirishaji wa majini kwa ajili ya Watanzania na nchi nyingine zinazotumia bandari za Tanzania. Moja ya bandari ambayo inaboreshwa kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na kujengwa gati la kisasa na eneo la kuhifadhia mizigo ni Bandari ya Mtwara. Katika mahojiano na gazeti hili hivi karibuni, Mkurugezi Mkuu ...

Read More »

Ndugu Rais, Willbrod Slaa ni balozi, padri mpinzani

Ndugu Rais, Watanzania wa leo wengi wana fikra nzito kuliko baadhi ya waheshimiwa. Nimetumiwa meseji mbili. Ya kwanza mwandishi anasema amesukumwa na makala yangu niliyoiandika miaka tisa iliyopita ikiwa na kichwa cha habari, “Rais wangu Kikwete kwaheri ya kuonana wapambanaji wetu.” Akaandika, “Kama ningalikuwa na uwezo wa kumfikia Mheshimiwa Rais ningemwambia neno moja. Nalo ni hili -wakati wenzako watakuwa na ...

Read More »

Tusipotoshe kauli tukaiharibu nchi

Siku ya Ijumaa ya Agosti 9, mwaka huu nilipigiwa simu na marafiki zangu wawili kwa nyakati tofauti na kutoka maeneo tofauti. Simu ya kwanza ilitoka maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam na simu ya pili ilitoka jijini Mwanza kule Usukumani. Katika simu zote mbili hizi ujumbe ulikuwa mmoja “…Brigedia Jenerali, umesoma gazeti [nalihifadhi] la Jumatano ya Agosti 7?” Niliwajibu wote ...

Read More »

Kiswahili kimepandishwa hadhi na SADC

Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Southern African Development Community, kwa Kiingereza, au SADC kwa kifupi), uliyomalizika Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, mwaka huu umeidhinisha matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya nne ya Jumuiya hiyo. Lugha nyingine rasmi za SADC ni Kiingereza, Kireno, na Kifaransa. Suala halikuwa ...

Read More »

Kwanini Bageni anyongwe peke yake kati ya watu 13?

Walioshitakiwa walikuwa 13, SP Christopher Bageni, ACP Abdallah Zombe, ASP Ahmed Makele, PC Noel Leornard, WP 4593 Jane Andrew, CPL Nyangerela Moris, PC Michael Shonza, CPL Abeneth Saro, DC Rashid Mahmoud Lema, CPL Emmanuel Mabura, CPL Felix Sandys Cedrick, CPL Rajab Hamis Bakari na CPL Festus Philipo Gwabisabi. Kwanini wameshitakiwa watu wote hawa halafu mtu mmoja ndiye aliyepatikana na hatia na akahukumiwa ...

Read More »

Ukipoteza muda, muda utakupoteza zaidi

Maisha huwa hayana maana iwapo mwanadamu anaishi tu, siku nenda, siku rudi bila ya kugundua au kujifunza japo jambo moja jipya kila siku. Uamkapo asubuhi, utembeapo barabarani, ulalapo kitandani yafaa ujiulize: ‘Unaishi na mawazo yanayoishi au yaliyokufa?’ Maisha ni kufikiri, binadamu wote tuna fursa ya kufikiri, haijalishi unafikiri nini, lakini unafikiri. Kinachotokea katika maisha yetu hakitokei nje ya kufikiri kwetu. ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (43)

Ukiomba mvua usilalamike kuhusu matope   Kulalamika ni mtihani. Unaweza kulalamika kuwa maua aina ya waridi yana miiba au kusifu kuwa miiba ina maua. Kuna mtoto aliyewalalamikia wazazi kuwa hawamnunulii viatu. Aliacha kulalamika alipoona mtu ambaye hana miguu, kuna makundi ya watu yanayolalamika kila mara: wale wasiopata wanachokistahili na wanaopata wanachokistahili. “Baadhi ya watu wanalalamika kila mara; kama wangezaliwa kwenye ...

Read More »

Tusibweteke kwa elimu bure

Julai 3, mwaka 1964 Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alizungumza na watoto katika Ikulu ya Dar es Salaam. Kupitia mazungumzo hayo, alizungumza pia na watoto wote nchini kwa njia ya redio. Aliwaeleza watoto wajibu walionao kwa wakati huo, ikiwa ni maandalizi ya wao wakiwa wakubwa kubeba mzigo mkubwa wa kuleta maendeleo ya taifa letu. Kama ilivyokuwa ada ya ...

Read More »

SADC inaweza, twendeni pamoja

Kuundwa kwa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) miaka 27 iliyopita ni kitendo cha ukombozi kwa Mwafrika. Ni ukombozi wa kisiasa, kiuchumi na kitamaduni. Unamtoa katika unyonge na umaskini na kumpeleka katika uwezo wa kuwa tajiri na kumiliki njia za uchumi kwa manufaa ya maendeleo yake katika jamii. SADC ina asili yake. Asili inayotokana na mawazo, ...

Read More »

Yah: Ugeni umetukumbusha mambo mengi

Japo ni vigumu kukubali maelezo ya sasa kutoka katika kizazi kipya, nina kila sababu ya kuwasimulia maisha halisi ambayo sisi tuliishi kwa wakati wetu, hasa nyakati za nguo moja na sabuni za foleni katika duka la ushirika au la kijiji. Leo dunia imebadilika sana. Kuna bomba kila mahali, kuna nguo lukuki, kuna mafuta ya kupaka, kuna usafiri, pia kuna unyunyu ...

Read More »

‘Konde Gang’ kuondoka WCB?

Msanii Rajab Abdul Kahali, maarufu kwa jina la ‘Harmonize, hatimaye ameandika rasmi kwa kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) akitaka kuvunja mkataba wake na kuanza maisha mengine nje ya lebo hiyo. Akizungumza na runinga ya Wasafi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa WCB, Sallam SK (alias Mendez) amesema msanii huyo ameandika rasmi kwa kundi hilo akisema anataka kujiondoa. Sallam amesema kwamba kwa ...

Read More »

Ona wachezaji TPL wanavyoburuzwa

Wakati Ligi Kuu imeanza rasmi, yapo mambo mengi ambayo yanatakiwa kutazamwa kwa undani na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Nalo ni suala linaloendelea kujirudia kila msimu, ambalo ni tatizo la wachezaji wengi kujikuta wakishindwa kutimiziwa yale yote ambayo wanaahidiwa kupitia mikataba wanayoingia na klabu. Uelewa wa wachezaji kuhusu haki zao za msingi wanazostahili kutimiziwa ndani ya kipindi wanachokuwa wakichezea timu ...

Read More »

Kashfa nzito

Serikali ya Rais John Pombe Magufuli imo hatarini kupoteza zaidi ya Sh bilioni 120 kutokana na mradi wa kukopesha matreka kwa wakulima ambao mkataba uliingiwa siku 8 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kugeuka ‘kichomi’, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Mkataba huo unaotajwa kuwa na mazonge mengi, uliingiwa Oktoba 22, 2015 ikiwa ni wiki moja na siku moja kabla ya ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons