TIMU ya Azam FC imeichapa bao 1-0 Singhida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Joseph Mahundi dakika ya 17 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mbaraka Yussuf.
Na sasa timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inafikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi ya 20, sasa ikizidiwa pointi mbili tu mabingwa watetezi, Yanga walio nafasi ya pili kwa pointi zao 40 za mechi 19, nyuma ya SImba wanaoongoza kwa pointi zao 46 za mechi 20.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, David Mwantika, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mbaraka Yusuph/Shaaban Iddi dk66, Yahya Zayed/Salmin Hoza dk90 na Joseph Mahundi/Ennock Atta Agyei dk30.
Singida United; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shafiq Batambuze, Miraj Adam, Salim Kipaga/Malik Antiri dk70, Kennedy Wilson, Kenny Ally, Deus Kaseke/Asad Juma dk66, Tafadzwa Kutinyu, Danny Usengimana, Kambale Salita na Kiggi Makassy.

2130 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!