Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi kombe kampteni wa timu ya Iringa United baada ya kuwafunga Mtwivila City kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi zawadi ya jezi kampteni wa timu ya Mtwivila baada ya kuwafungwa na timu ya Iringa United kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja

mashabiki na viongozi wa timu ya Iringa United wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga timu ngumu ya Mtwivila City kwa njia ya mikuju ya penati na kuwa wawakilishi wa mkoa wa Iringa kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi pesa na zawadi mchezaji bora wa mashindano Razack Kibuga ambaye ametoka katika timu ya Iringa United
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi pesa na zawadi golikipa bora wa mashindano Nelly Mkakilwa ambaye ametoka katika timu ya Iringa United
Baadhi ya wadau na mpira wa mikuu mkoani Iringa wakiwa wapo sambamba na kiongozi wa Iringa United walipokuwa wakifuatilia kwa ukaribu mechi katika ya Iringa United na Mtwivila City kutoka kushoto anaitwa Frank Lyimo kutoka kituo cha TV cha IMTV ,Ally Msigwa ambanye ni mkurugezi mtendaji wa Iringa Football Academy na anayefuata ni Steve Lihawa mtangazaji wa kipindi cha michezo cha radio Ebony fm iliyopo mkoani Iringa

TIMU ya Soka ya Iringa United imefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Mkoa wa Iringa baada ya kuibuka na ushindi penati 3 – 1 dhidi ya Mtwivila Fc.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Samora timu ya Mtwivila Fc walikuwa wa kwanza kupata bao dk 8 kupitia kwa mshambuliaji hatari David Mwanga baada uzembe wa golikipa wa Iringa United Nelly Mkakilwa kuponyokwa na mpira na kumpita tobo.

Mchezo huo uliokuwa wa kukamiana mwanzo mwisho huku baadhi ya wachezaji wakionyesha ufundi mwingi wa kuchezea mpira hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtwivila walikuwa wakiongoza bao 1.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kuonyesha kuwa hawajabahatisha kufika fainali ya ligi ya Mkoa kwa Mtwivila wakitaka kuongeza huku Iringa wakitaka kurudisha.Mchezaji bora wa mechi ya nusu fainali Razack Kibuga aliibuka shujaa baada ya kusawazisha goli katika dk 76 na kuwaacha wachezaji wa Mtwivila wakilaumiana.

Mara ya dakika 90 kumalizika ndipo hatua za kupigiana matuta ilipowadia ambapo timu ya Mtwivila fc ilikosa penati 3 na Iringa United kupata penati 3 dhidi ya 1. Kutokana na ushindi huo timu ya Iringa United imejinyakulia jezi seti moja, mipira miwili huku timu ya Mtwivila wakiondoka na jezi na mpira mmoja.Mchezaji bora wa mashindano hayo aliibuka Razack Kibuga wa Iringa United aliyeondoka na zawadi ya sh.100,000 na cheti golikipa bora alikuwa Nelly Mkakilwa toka Iringa United aliyepata sh.50000

Katika mchezo huo mgeni rasmi alikuwa mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa soka Mkoani hapa Feisal Abri Asas ambaye alikabidhi kombe la ubingwa kwa nahodha wa Iringa united, Ahmed Kivike.Akizungumza kabla ya kukabidhi kombe hilo Feisal alisema kuwa anatarajia kudhamini ligi ya Mkoa mwakani kwa kuwa mwaka huu yamekuwa na mafanikio makubwa.

Wakati huo huo ya soka ya Mkimbizi fc imefanikiwa kushika nafasi ya tatu ya ligi ya mkoa baada ya kuwafunga timu ya soka ya Mshindo fc mabao 5 – 4.Katika mchezo huo mkali uliopigwa majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Samora timu ya Mshindo ‘wabishi wa mjini’ itabidi wajilaumu kwa kuwa hadi kipindi cha kwanza walikuwa wanaongoza goli 3 – 2 kwa magoli yaliyofungwa na Michael Chader dk za 8,17 na 23.

Magoli ya Mkimbizi fc yalifungwa na Said Kaliumi aliyefunga magoli matatu katika dk za 10 na 29 na 53.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Mshindo Fc kufunga goli la nne kupitia Michael Chader katika dk 50 lililodumu hadi dk ya 53 ambapo Mkimbizi Fc walijipatia goli kupitia kwa Said Kaliumi.Mkimbizi Fc wakiwa nyuma kwa goli mbili walikuja kwa kasi na kuanza kufunga katika dk za 64 na 70 na kufanya matokeo kuwa 5 – 4

Kwa ushindi timu ya mkimbizi imefanikiwa kuwa Mshindi wa tatu katika ligi ya Mkoa na kuondoka na zawadi ya jezi seti moja.

By Jamhuri