Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb.), amewasili Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja-Zanzibar, ambapo ni mgeni rasmi katika Mdahalo wa Nishati Safi unaolenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu nishati hiyo, leo tarehe 11 Agosti 2026.

Mdahalo huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali na wadau kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Kutoka Wizara ya Nishati, Waziri Ndejembi ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb.), Katibu Mkuu (Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Felchesmi Mramba, pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati.

Mdahalo wa Nishati Safi umeandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation, ambayo Mwenyekiti wake ni Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ambaye ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mdahalo huo umeambatana na Maonesho ya wadau wa nishati safi ya kupikia waliohudhuria Mdahalo wa Nishati Safi, unaofanyika katika Hoteli ya Kwanza-Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja-Zanzibar.