Mshambuliaji wa timu ya soka ya Manchester City, Mario Balotelli (22), yupo mbioni kuhamia AC Milan.

Tayari mchezaji huyo amekamilisha maandalizi ya kujiunga na AC Milan kwa mkataba wenye thamani ya dola milioni 24.


Balotelli amesema ameshatoa taarifa za nyumba yake ya kupanga huko Cheshire na ameanza kusafirisha mali zake kuelekea AC Milan.


Wiki iliyopita, mwakilishi wake, Mino Raiola, alikuwa nchini Italia kwa mazungumzo ya kurejea San Siro.


Meneja wa Klabu ya Manchester City, Roberto Mancini, amefurahishwa na hatua ya mchezaji huyo kurejea AC Milan.


5144 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!