Madini yasichimbwe hovyo hovyo

Dhahabu ni Tanzanite, almasi na mali asilia nyingine nyingi huwa vinawekwa benki kuu kama sehemu ya fedha wanauchumi wananielewa Nyerere aliamua bidhaa kama hizi zisichimbwe hovyo hovyo benki kuu yake vibakie humo humo ardhi kwa kizazi cha baadae. Vipi wewe na mini unadhani tunanufaika kwa vyoyote vile na hizi bidhaa sasa zinachimbwa hovyo tokea Watanzania tusike kelele za gesi haijapita hata nusu mwaka tayari washasimika mabomba ya kuvuna Kuna uraniamu kule Singida nayo wanaifanyia mikakati ya kuichimba bila ya kuzingatia madhara ya kiafya itokanayo na uraniamu kwa kuzingatia kwamba hatuna wataalumu wazawa wa kutukinga mambo haya madhara ya uraniamu ni makubwa kuliko ukimwi.

0765441474

Hatuna muuguzi wa zahanati

Sisi wa kazi wa Tarafa ya kwa Mtoro Kata ya Lalta Kijiji cha Magambua tumekuwa na tukipata shida sana kwenye huduma za kijamii maji kama afya matatizo ambayo yameshindwa kupatiwa uvumbuzi Zahanati ya Magambua ina mwezi haina muhudumu wananchi wakienda wanambiwa muuguzi yuko likizo juzi kuna mama alipata uchungu wa kujifungua lakini alipofika pale alikuta kumefungwa akajifungulia mlangoni pia katika Kijiji cha Ilasee  wamama wanalala nje kwa ajili ya kutafuta maji tunajiuliza ni nani takayesilikiliza kilio chetu tusaidiwe pia tunalazimishwa kujinga na mfuko wa matibabu (NIHF)

0765141939

 

JAMHURI limetufumbua macho

Nawapongeza na kuwapa pole wana JAMHURI. Ni kweli vitisho vipo na vitazidi kuja, ila Watanzania wengi tuko nyuma yenu. Mtambue kuwa kugusa mfumo (corrupt syndicate) si lelemama. Watanzania wengi gazeti hili limetufumbua macho. Niwaombe Watanzania wenye nia njema tuzidi kumwomba Mungu ili ukweli uendelee kushinda.

Albert Mwombe (ADVOCATE), Lindi

0688 405 748

Serikali imekosea kuzuia daladala

Uwanja wa maoni mzuri sana kipindi kile daladala zinapigwa marufuku pale Dar es Salaam kwa kisingizio cha kupunguza foleni niliona ni jinsi serikali yetu ilivyooza dhaifu kwani moja wapo ya tabia ya nchi inayoongozwa kijamaa (Communism) ni magari ya mizigo na yale ya kuihudumia jamii mengi au yanakuwa yametawala kuliko magari binafsi hivyo basi sikuona mantiki ya daladala kupigwa marufuku badala yake` wamegeuzia magari binafsi kuingia mjini nilikosa pa kulisemea hili sasa nimepata upeo mapana.

0765441474

 

Chadema malizeni tofauti zenu

Jamani Chadema malizeni tofauti zenu Watanzania tumeweka  matumaini yetu kwenu ili muikomboe nchi hii msituangushe chonde chonde jamani.

Julius Nyamwihura, Bukoba

0754830350

 

Lowassa anafaa kuwa rais

Watanzania  wengi hawaoni mbalia isipokuwa wao wanapoona mtu anachafuliwa tu kwa saisa kufisadi na kadharika basi hafai si kweli ukinagalia kwa uapana kama tutaka maeandeleo ya haraka katika nchi hii basi huyui ndugu Lowassa anaweza akaleta maajabu si muoga wa maamuzi kiongozi unatakiwa uwe hivyo masomaji nwa jamhuri.

0712746331

 

Ukiukaji wa haki za binadamu

Ukiukwaji wa haki za binadamu  uliofanywa nchini Sri Lanka, umesababisha Mauritus kujiondoa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Jumuiya hiyo mwaka  2015.

0764 940 171

 

Mbowe, Zitto wanatuulia chama

Mie ni mwanachama wa Chadema ambaye sikujiunga na chama kwa kufuata mtu bali sera nzuri za chama nionavyo mimi viongozi hawa  wamekusudia kutuulia chama mawazo yangu.  Mbowe na Zitto wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote ndani ya chama wala watu wanaonekana kukoleza mgogoro nao wasiruhusiwe Ila waruhusiwe kutetea majimbo yao.

0785055439

1371 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!